Na,Nishan khamis.
Mkoa wa kaskazini Unguja.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe,Mattar Zahor Masoud ameipongeza ofisi ya mrajisi wa asasa za kiraia kwa kuona umuhimu wa kuwapatia elimu masheha wa mkoa huo katika uelewa wa usajili na usimamiza wa asasa hizo katika maeneo yao hasa kipindi hichi tunacho elekea cha uchaguzi mkuu wa serikali 2025.
Mhe, Mattar ameyaemea hayo leo huko mkokotoni wilaya ya kaskazini A Unguja ofisini kwake wakati akifungua mafunzo hayo ya siku moja kwa masheha wa mkoa huo juu ya uelewa wa usajili na usimamiza wa asasi za kiraia zilizopo katika mkoa huo.
Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi linathamini kwa kiasi kikubwa mchango wa asasi za kiraia katika kuisadia serikali katika masuala mbali mbali ya kimaendeleo nchini.
RC,Mattar amewataka masheha kuzingatia elimu hiyo kwa misingi ya kuendelea kushirikiana katika kueleta maendeleo zaidi huku akiwataka kuziripoti asasa zote zitakazo kwenda kinyume na zenye nia mbaya na nchi hasa kipindi hichi kuelekea uchaguzi mkuuu nchini 2025.
Mrajis wa jumuiya zisizo za kiserikali Ahmed Khalid Abdulla awali akimkarabisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa huo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo masheha wa mkoa huo katika kutambua usimamiza wa asasi za kiraia katika shehia zao kwani usajili wa asasi hizo lazima taratibu zianze ngazi ya shehia,wilaya mpaka kufika kwa mrajisi wa asasi hizo.
Mrajisi amesema asasi zina mchango mkubwa katika kuisadia sereikali katika masuala mbali mbali ya utatuzi wa changamoto za jamii na kuendelea kashirikiana na serikali katika kuimasha maendeleo nchini.
Amewasisistiza masheha kuwa makini kwani kilindi tunacho elekea uchaguzi historia inaonyesha baadhi ya asasi hukiuka kanuni na katiba za asasi hizo na kufanya majukumu ma kazi kinyume na sheria na taratibi za asasi,amewataka masheha asasi yoyote itakayo kiuka utaratibu katika maenoe yao ziripotiwe kwa hatua zaidi zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wao masheha wamesema elimu waliyoipata imewaelimisha kwa kiasi kikubwa katika kuwaletea kufanya kazi zao kwa ufasi zaidi kwani awali mambo mengi walikuwa hawayatambui kuhusu maswala ya taratibu za asasi za kiraia.
Hivyo wameahidi kuzingatia na kuyafanyia kazi mafunzo hayo kwa misingi ya kuonesha mashirikiano kwa maendeleoa ya shehia zao,mkoa na taifa kwa ujumla.

