Fukuchani wilaya ya kaskazini A Unguja.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema Uwekezaji unaoendelea nchini katika sekta ya utalii ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na maono ya rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar Dkt Husein Ali Mwinyi katika kuongeza pato la taifa ikiwa ni matunda ya mapinduzi ya mwaka 1964.
Mhe, Mazrui ameyaema hayo leo katika kijiji cha Fukuchani ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa mradi wa villa za heritage sunset retreat Zanzibar Fukuchani wilaya ya kaskazini A Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya zanzibar.
Amesema mradi huo unaumuhimu mkubwa kwa jamii ya Fukuchani na taifa kwa ujumla katika kutia ajira na kukuza uchumi wa taifa ikiwa eneo hilo lina umuhimu mkubwa wa kihistoria Zanzibar.
Aidha amesema kutokana na umuhimu wa mradi huo na historia ya eneo hilo ametoa wito kwa wizara kuendelea kufanya utafiti zaidi na kuyakarabati maeneo mbali mbali ya kihistoria ili yawavutie zaidi wawekezaji waliopo nchini na nje ya nchi kuwekeza zaidi kwa maendeleo ya taifa.
Aidha amewasisitiza wanakijiji hicho kuendelea kuunga mkono juhudi za rais na kushirikiana na wawekezaji katika kuleta maendeleo zaidi nchini huku akiwahamasisha vijana kusoma zaidi ili kufanya kazi za kitalii kwa weledi zaidi katika sekta hiyo.
Akisoma taarifa ya kitaalamu kwa niaba ya katibu mkuu wizara ya utalii na mambo ya kale Naibu katibu mkuu wizara hiyo Dkt Amina Ameir Issa amesema eneo hilo ni eneo la kihistoria ambapo mwaka 1600 eneo hilo lilikuwa ni eneo la kibishara kwa wareno na kupitia ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM 2020-2025 pamoja na dira ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Dkt Amina amesema ujenzi huo ulianza mwaka 2023 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2025 ambapo mpaka sasa asilimia 40 umekamlika na mpka kukamilika kwake itagharimu kiasi cha Dola milioni mbili za kimarekani .
Kwa upande wake mwekezaji wa mradi huo balozi wa heshima wa Ufaransa ndugu Yves Montel amesema ameishukuru wizara pamoja na wanakijiji cha Fukuchani kwa ushirikiano wao katika mradi huo pamoja na kuuunga mkono juhudi za serikali kwa wawekezaji jambo ambalo limekuwa na msaada mkubwa katika kuendelea kuwekeza zanzibar.
Yves amesema katika ujenzi wa mradi huo wamezingatia Kuhifadhi eneo la kihistoria pasi la kuligusa kwani lina umuhimu mkubwa wa kihistoria katika kijiji hicho huku akiwahidi vijana kuwapa ajira na kutoa nafasi za masomo ya utalii kwa vijana wa Fukuchani ili wanufaike na Uwekezaji katika kijiji chao.
Akitoa salam za mkoa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja mkuu wa wilaya ya kaskazini A Unguja Ndugu Rashid Simai Msaraka amesema mkoa huo upo salama,amani na utulivu jambo ambalo linachochea maendeleo zaidi katika wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.
Msaraka amesema mkoa huo umenufaika kwa kiasi kikubwa na sera ya utalii kutoka na jitihada za Dkt Mwinyi za kimaendeleo za wilaya na mkoa huo ni jambo la kupongezwa na kuunga mkono kwa viongozi wote nchini kwa kazi nzuri za kuwatumikia wananchi.