Na,Nishan khamis.
Wilaya ya kaskazini A Unguja.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Kaskazini Unguja ndugu Idi Ali Ame amempongeza waziri wa afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui kwa usimamizi mzuri wa kusimamia ilani ya CCM 2020-2025 katika sekta ya afya nchini.
Mwenyekiti ametoa pongezi izo hapo jana katika sherehe za ufunguzi wa mradi wa villa za heritage sunset retreat Zanzibar Fukuchani wilaya ya kaskazini A Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 61ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema katika mkoa huo anajivunia uwepo wa hospital za wiliya za kisasa, vituo vya afya na hospital ya mkoa inayoendelea kujengwa Mahonda pamoja na vifaa vya kisasa na huduma bora zilizopo ni ni jambo la kupongeza waziri kwa kazi kubwa ya kumsaidia rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt Husein Ali Mwinyi kwa jitihada anazo fanya katika kuimarisha miundombinu bora ya afya nchini ikiwa ni ahadi yake katika kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Hivyo amewanasihi wananchi wa Fukuchani na mkoa huo kwa ujumla kumuunga mkono Dkt Mwinyi na Dkt Samia kutokana na jitihada kubwa wanazo zifanya za kimaendeleo nchni na ikifika oktoba mwaka huu zote kwa marais hao.

