Popular services

MVIWATA WAADHIMISHA MIAKA 61 YA MAPINDUZI KWA kUPANDA MPUNGA BONDE LA KILOMBERO

Na,Nishan khamis. 

Mkoa wa kaskazini Unguja. 

Mtandao wa wakulima wadogo wadogo Tanzania(MVIWATA) kanda Ya Zanzibar leo wameadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujumuika pamoja na kupanda mpunga katika bonde la mpunga kilombero wilaya ya kaskazini B Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo mwenyekiti wa MVIWATA kanda ya Zanzibar Hadia Ali Makame amesema mtandao huo unatambua na kuunga mkono Mapinduzi ya mwaka 1964 ambapo muhasisi wa Mapinduzi hayo Sheikh Abeid Amani Karume alisisitiza sana juu ya kilimo nchini hivyo wameamua leo kuyaasisi Mapinduzi hayo kwa kujumuika na kupanda mpunga kwa pamoja kutokana na umuhimu mkubwa wa kilimo ambapo maendeleo makubwa yamepatikana kwa wakulima kipindi cha miaka 61 ya mapinduzi Zanzibar. 

Hadia amesema maadhimisho hayo yamefanyika na shughuli wanayoifanya kwani mapinduzi ya Zanzibar yamekuja kumkomboa mkulima hivyo ameitaka jamii kufanya uchechemuzi katika kuyatunza maeneo ya kilimo pamoja na kutumia kilimo chenye tija kwa maendeleo ya mviwata na taifa kwa ujumla.

Aidha ameiomba serikali kuangalia na kudhibiti matataizo mbali mabli ya maeneo ya wakulima ili waweze kuwa na maeneo makubwa yenye uzalishaji bora na mkibwa wa mawzao nchini.

Mkurungezi mtendaji wa bodi ya wadhamini Mviwata taifa Namri Najm Jecha amesema mapinduzi yalikuwa na lengo na dhamira la kumkomboa mkuklima ambapo Shekih Abeid karume aliwapa kipaumbele wakulima na alifanya ukombozi ili wakulima wawe na amani na utulivu pomoja na kuwapatia ekari 3 kila mkulima ili wanufaike na shuguli zao za uzalishaji wa mazao nchini.

Namri amesema mviwata kazi kubwa ni kufanya utetezi na ushawishi kwa wakulima kwa maendeleo zaidi hivyo wanatoa pongezi za dhati kwa serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na rais wa serikali ya mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha miundo mbinu ambayo imekuwa na tija kwa wakulima kwa maendeleo ya kilimo nchini.


Kwa upande wao baadhi ya wakulima wamesema licha ya mafanikio yaliyopo katika mtandao huo lakini uwepo wa uchakavu wa matrekta,mifugo kuharibu mazao pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa zinazo rejesha kufikia malengo ya wakulima wadogo wadogo nchini. 


Tatu Juma Rubisha ni miongoni mwa wanachama wa mviwata kanda ya Unguja akitokoea wilaya ya Magharibi A Unguja amesema kwa upande wake anajishughulisha na kilimo ufugaji ambapo amenufaika kwa kiasi kikubwa kawepo katika mtandao wa mviwata kwani aneweza kusomesha watoto wake,kujikimu kimaisha pamoja na kupata soko la uhakika hotelini,masokoni na mtu mmoja mmoja kutokana na uuzaji wake wa kuku ikiwa ni shughuli yale inayo muingizia kipato kutokana na kilimo ufunguzi wa kisasa elimu amabayo anajivunia kuipata tangu kujiunga na mtandao huo.

Amewashauri wanawake kutumia fursa za kilimo cha mazao na ufugaji kwani vina tija katika kumkomboa kiuchumi mwanamke na kuweza kuacha utegemezi wa nyumbani jambo amabalo baadhi ya wanawake wanadhalilika kutoka na ukosefu wa shughuli za kufanya. 

Nae Ali Maabad Omar ni miongoni mwa wanachama wa mviwata kutokea wilaya ya kaskazini B Unguja amesema licha ubodreshwaji wa miundo mbinu katika kuwasaidia wakulima lakini kuwa uapande wa wilaya yake wanakabiliwa na changamoto za uchakavu wa trekta na mifungo kuingia mashambani ni changamoto kubwa zinazo rejesha nyuma katika zitihada zao za kilimo.