Popular services

MMOJA AFARIKI BAADA YA KUJERUHIWA NA WATU WASIO JULIKANA MUANGE


Na,Nishan khamis
Mkoa wa kaskazini Unguja.

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina Machu Silima Khamis miaka 22 mtumbatu mkaazi wa shehia ya Muange wilaya ya kaskazini A Unguja Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 26 Januari 2025 majira ya saa kumi jioni aliokotwa barabarani huko shehia ya Muange  na wasamalia wema wakati mwili wake ukiwa na majeraha mgongoni ambapo wasamalia wema hao walimchukua na kumpeleka nyumbani kwao.
Hayo ameyasema kwa njia ya simu  kamishina Msaidizi mwandamizi Benedict Mapujila kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Unguja akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi,amesema tukio hilo la mauwaji limetokea hapo jana na marehemu aliokotwa  akiwa na majeraha sehemu za mgongoni na kupelekwa nyumbani kwao na badae katika hospital ya kivunge ambapo mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakija julikana wala wafanyaji wa tukio hilo hawaja julikana na shauri hilo linaendelea na upelelezi zaidi kubaini chanza na wafanyaji wa tukio hilo.

Kamanda Benedict ametoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia hatua mkononi na kuacha vitendo vya kihalifu huku akito msisitizo wa kuendelea kushirikiana na kushikamana katika kutokomeza vitendo vya kihalifu katika mkoa huo kwa kuendelea kutunza amani,utulivu upendo uliopo nchini ambapo mwili wa marehemu ulikabidhiwa hapo jana kwa ndugu zake kwa utaratibu wa mazishi zaidi.

Akithitibisha kupokea mwili wa marehemu hapo jana  Daktari zamana hospital ya wilaya Kivunge Daktari Haji Machano Haji amesema waliopokea mwili huo hapo jana majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni marehemu akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha sehemu za mgongoni na baada ya uchunguzi wamebaini alichoma na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kupelekea kifo cha marehemu huyo.

Kwa upande shaha wa shehia ya Muange Mcha Idi Haji amesema mara baada ya kupata simu kuhusu tukio hilo alifika nyumbani kwa marehemu na kujumuika na ndugu na badae kumpelekea marehemu Hospital ya Kivunge kwa uchunguzi zaidi ambapo alisema amesikititishwa na tukio hilo, na amesema hajafanikiwa kutambua chanzo cha  tukio hilo hivyo atahakikisha anashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na jamii kwa ujumla ili  kubaini chanzo cha tukio hilo na wafanyaki wa tukio na sheria ichukue mkondo wake   kwa watakao bainika juu ya tukio hilo.

Nae ndugu wa marehemu Ali Haji Khamis amesema kwa niaba ya familia wamepokea kwa masikitiko makubwa kwa tukio hilo na waiomba serikali iendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo na wafanyaji wa tukio hilo kuchukuliwa hatua za kisheria.