Na,Nishan khamis.
Mkoa wa kaskazini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amemkabidhi bendera Kiongozi wa Matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar ( UVCCM )Komred Juma Usonge amabe pia ni mbunge wa jimbo la Chaani kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi nikiashiria Uzinduzi wa Matembezi ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Katika Uwanja wa Mpira wa Tumaini Mkwajuni, wilaya ya kaskazini A Unguja Mkoa wa Kaskazini Unguja na kupitia katika Wilaya na Mikoa yote ya Unguja na Pemba.
Mhe, Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar ( UVCCM ) kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Uzinduzi wa Matembezi ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Katika Uwanja wa Mpira wa Tumaini Mkwajuni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema katika kujenga nchi yenye maendeleo ni lazima kuwepo na misingi Imara itakayolisaidia Taifa kufikia malengo yake, ni lazima jamii iweze kuepukana na vitendo viovu vya dhulma, chuki, rushwa na ufisadi kwa mustakbali mwema wa vizazi vya sasa na baadae.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema vijana watakaposhikamana vizuri na kusaidiana katika kutafuta na kutengeneza ajira wanaweza kutatua kwa kiwango kikubwa changamoto mbali mbali za kimaendelo zinazoikumba jamii katika kufikia Mapinduzi ya kiuchumi na kimaendelo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Comred MOHAMED ALI KAWAIDA amesema watahakikisha watayatumia matembezi hayo kwa kuwahamasisha Vijana na wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili Chama cha Mapinduzi kiweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025 ili CCM iendelea kushika Dola.
Kwa upwnde wake Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM anaefanyia kazi zake Zanzibar Ndugu ABDI MAHMOUD ABDI amesema Matembezi hayo yatakayojumuisha vijana zaidi ya Elfu nne(4000) yana lengo la kuadhimisha Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar amabayo yameifanya zanzibar kuwa nchi yenye na Amani na Utulivu.
Matembezi hayo yaliyozinduliwa leo yatapita katika Mikoa na Wilaya zote za Unguja na Pemba ambayo yanatarajiwa kufikia kikomo Januari 10, 2025 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba na kufungwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.



