Popular services

WANAFUNZI SUZA WAWAFARIJI WATOTO YATIMA NA WAGONJWA HOSPITAL YA KIVUNGE


Na,Nishan khamis. 

Wilaya ya Kaskazini A Unguja. 

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Zanzibar(SUZA) kampasi ya Chwaka kwa kushirikiana na taasisi ya Global Youth empowerment ya Dar es Salaam leo wamefika katika shehia ya mkwajuni na kivinge zilizopo wilaya ya kaskazini A Unguja na kukutana na watoto yatima,wenye mazingira magumu pamoja na kupata wasaa wa kufanya usafi hospital ya Kivunge na kuwatembelea wagonjwa katika hospital hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa Zanzibar Student  Charity-Sob Chwaka Latifa Omar Mwinyimkuu amesema lengo la safari hiyo ni kuwapa chochote watoto hao na kuwapa  hamasa watoto watoto hao katika kufanya jitihada za kusoma ili kubadilisha mazingira yao na kuweza kufika ndoto zao za maisha.


Lailat amesema watoto yatima na wenye mazingira magumuu wanapitia changamoto mbali mbali katika kuzifikia ndoto zao hivyo Zanzibar Student Charity wameliona hilo na kujihamasisha wanafunzi wa vyuo katika kutoa msaada kwa wadogo zao ili waweze kuyafikia malengo yao kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Amesema zaidi ya watoto mia moja wmaekutana nao leo na kufarajika nao pamoja na kuwapa msaada kidogo wa vifaa vya skuli ili viwasaidie katika kipindi cha skuli zikifunguliwa wajione wenye faraja kama watoto wengine ambapo mpaka sasa wamefanya zoezi hilo mara mbili na kuahidi kuendelea nao kwa misingi ya kuwahamsisha watoto hao nchini.

Pia amesema wamepata nafasi ya kufanya usafi hospital ya wilaya Kivunge na kuwaona wagonjwa   na kuwafariji jambo ambalo lina umuhimu mkubwa katika jamii hasa kwa vijana.

Aidha emebainisha ukosefu wa kifedha ndio changamoto kubwa kwao hivyo ameomba serikali,taasisi mbali mbali pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kwasaidia watoto wa aina hiyo hapa nchini ila nawao waweze kuyafikia yale malengo yao .

Mkurugenzi wa Global Youth Empowerment kutoka Dar es Salaam Amina Sanga amesema katika kuwapa hamasa watoto ameamua kushirikiana na Zanzibar Student Charity katika ziara hiyo na kujumuika pamoja katika harakati za kijamii kwani vijana wanawajibu mkubwa katika harakati mbali mbali za kijamii nchini.

Amewapongeza vijana hao na kuwaomba wengine kujitoa katika kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu kwani kupitia ziara hiyo ameona uwezo mkubwa kwa watoto wenye mazingira magumu hivyo jitihada kubwa zikiekezwa zitawajenga watoto hao kutimiza ndoto zao na kuja kuwa viongozi bora hapo badae.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi sheha wa shehia ya Kivunge Huwen Haji Juma na Jumbe Idd Jumbe sheha wa shehia ya Mkwajuni wamewapongeza ujio huo kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuwapa hamasa watoto na kujumuika katika shuguli za kijamii ni jambo la kuungwa mkono na kuendelea kutekeleza yale yanayo himizwa na viongozi nchini katika uwajibikaji wa vijana katika maendeleo ya nchi.

Masheha hao wametoa wito kwa vijana wengine,taasisi mbali mbali na wadau kuendelea kuwaona watoto yatima na wenye mahitaji maalumu kuwasaidia watoto ili waweze kuyafikia malengo yao kwa mabadiliko yao na taifa kwa ujumla nchini. 

Nao watoto wamesema wamefurahishwa na ujio wa wageni kwani imawapa hamasa zaidi katika kusoma kwa kuzingatia utii,nidhamu na juhudi ikiwa ndio kuu za kufikia malengo yao,hivyo wameomba kuendelea na moyo huo wenye umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya watoto hao.