Na,Nishan khamis.
Mkoa wa Kusini Pemba
Mjumbe wa baraza kuu mkoa kusini pemba na mjumbe wa kamati ya utekelezaji baraza kuu Taifa ambae pia Katibu Tawala Wilaya Kaskazini "A" Unguja Bi. Maryam Said Khamis amewataka Wazazi na Walezi wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba kuendelea kuwapa ushirikiano wa karibu walimu ili kufanikisha Maendeleo mazuri ya elimu kwa watoto wao.
Amesema uwepo kwa Mashirikiano mazuri kwa Wazazi na Walimu itawasaidia wanafunzi wa skuli ya Msingi Kengeja kupata uelewa mzuri pamoja na kuongeza idadi ya ufaulu kwa wanafunzi ikiwa ni msingi mzuri wa kuunga mkono juhudi za rais Dkt Husein Ali Mwinyi rais wa Zanzibar na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kielimu wanazo zifanya nchini.
Maryam ameyasema hayo hapo jana alipo tembelea skuli ya msingi Kengeja wilaya ya mkoani mkoa wa Kusini Pemba na kukaabidhi Mashine moja ya Photocopy yenye thamani ya shilingi Milioni Saba ikiwa ni ahadi yake aliyoiweka mara baada ya kupata taarifa ya changamoto hiyo katika skuli hiyo.
Hivyo ametoa wito kwa uongozi wa skuli kuitunza na kuitumia kwa malengo yanayo hitajika ili idumu kwa muda mrefu na kuendelea kutoa huduma mbali mbali za kiofisi kwa maendeleo ya skuli hiyo.
Nae, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Kengeja Mwalimu Omar Ali Omar amesema uwepo wa Mashine ya Photocopy itawasaidia katika kufanikisha shughuli zao na kupunguza gharama za utoaji wa mitihani ya Wanafunzi nje ya ofisi za skuli pamoja kuahidi kuitunza Mashine hiyo.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa U.W.T Wilaya ya Mkoani Bi. Maryam Matora Husein amempongeza Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Baraza Kuu U.W.T Taifa kwa kutimiza ahadi yake kwa Walimu amesema hiyo ndio tabia ya kiongozi bora kutimiza ahadi zake kwa wananchi.