Popular services

MNEC NADRA ATOA M.5 NA CHARAHANI 10 KWA UWT MKOA WA KUSINI PEMBA



Pemba.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa anaye wakilisha wanawake mkoa wa Kusini Pemba Nadra Gulam Rashid leo amekabidhi charahani 10 na amechangia kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za  UWT ikiwa ni agizo amelitoa  mwenyekiti wa UWT katika kuimarisha maendeleo ya jumuiya hiyo.

Akizungumza na UWT mkoa huo amesema dhumuni la  ujio wake ni mwendelezo wa viongozi wa UWT taifa katika kuwahamasisha wanawake kujenga nyumba za jumuiya amabazo zitakuwa na mchango mkubwa katika kuandaa mikakati madhubuti ya maendeleo ya jumuiya kwa maslahi ya wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kufanya siasa safi na kuzikimbilia fursa mbalimbali za uongozi nchini.

Nadra amewataka wanawake kuanzisha baishara ndogo ndogo ambazo zitawasaidia katika kujikwamua kiuchumi kwani wanawake wakiwa na uchumi bora utawasadia katika kushiriki ipasavyo kwenye kuzikimbilia fursa za uongozi na kujiimarisha kiuchumi kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anavyo wanyanyua wanawake kiuchumi ni jambo la kumuunga mkono na kuoensha juhudi zaidi katika hilo.

Nae mwenyekiti wa UWT mkoa huo Zuwena Abdalla Haji ametoa pongezi za dhati kwa MNEC Dadra kwa jitihada anazo fanya katika mkoa ambapo amesema amepokea shilingi milioni 5 kwa ajili ya uchangiaji wa jengo la UWT, charahani 10 kwa kila wilaya ya UWT charahani tano na kiasi cha shilingi milioni moja ikiwa ni fedha zitakazo wasaidia katika kuanzisha shughuli zao hizo ni jambo la kuungwa mkono viongozi hao katika kuendelea kuleta mabadiliko zaidi ya maendeleo kwa wanawake nchini.