Popular services

ZASFICU YAWANOA WAANDAMIZI WAKE, WATOA PONGEZI KWA DKT MWINYI


Na,Nishan khamis
Zanzibar.

Chama cha ushirika cha wavuvi wadogo wadogo Zanzibar(ZASFICU) jana kilihitimisha mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo waandamizi 24 wa Zasficu,mafunzo hayo yalifanyika katika hotel ya Golden Tulip Airport Mkoa wa Mjini Magharibi kwa ufadhili wa WIOMSA-ZANZIBAR.

Akifunga mafunzo hayo Mhe, Moh'd Sudi Moh'd kwa niaba ya mkurungezi wa idara ya maendeleo ya uvuvi na mazao ya baharini Zanzibar amesema mafunzo hayo kwa washiriki yanatija kubwa kwa kuleta ufanisi kwa watendaji wa zasficu katika kukuza sekta ya uchumi wa buluu kupitia uvuvi hivyo ni vyema mafunzo hayo wakayaendeleza kwa maslahi bora ya zasficu na taifa kwa ujumla.

Mhe,Moh'd amewapongeza wafadhili wa mradi huo pamoja za washiriki wa mafunzo hayo pamoja na jitihada kubwa wanazo fanya zasficu na kuwahidi kuendelea kushirikiana nao katika nyanza zote huku akiwanasihi wavuvi kuacha uvuvi wa zamani na kufanya uvuvi wa kileo cha maslahi mapana ya wavuvi na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa zasficu Maalim Omar Moh'd Ali awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema zasficu inampongeza kwa kiaisi kikubwa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt Husein Ali Mwinyi kwa mchango wake mkubwa katika chama hicho na misingi aliyoweka ya kimaendeleo katika kuwainua kiuchumi wavuvi wadogo wadogo nchini.

Maalim Omar amesema suala la elimu ni jambo kubwa hivyo ikiwa yeye ni dhamani wa zasficu atahakikisha anasimamia ipasavyo mafunzo hayo kwa misingi ya kuleta maendeleo kwa wavuvi wadogo wadogo nchini ili kuwa na maendeleo bora kutokana na shughuli zao wanazo fanya hata hivyo ametoa shukran za dhati wizara ya uchumi wa buluu kwa ushirikianao wapo pamoja na wafadhali wa mradi huo wiomsa kwa kuona umuhimu mkubwa wa ufadhili wa mafunzo hayo.

Mkurugenzi mtendaji wa WIOMSA-ZANZ ndugu Arthor Tuda  amesema amewapongeza waandamizi wa zasficu kwa fursa hiyo na amewahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuboresha hali ya uchumi wa bahari ili kuleta matumizi bora ya Sayansi ya bahari kwa kukuza maisha bora ya wavuvi wadogo wadogo Zanzibar.
Kwa upande wake Almas Moh'd kutoka zasficu akionesha mpango kazi wa chama hicho mwaka 2025 amesema lengo kuu la zasficu ni kukuza uwezo wa wavuvi wadogo wadogo wa Zanzibar ili kufika ustawi wa uchumi na kijamii.

Nae, Rahma Khatib Mgeni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiaisi kikubwa katika kuongeza taasisi yao kwa weledi na ufanisi zaidi kwa Maslahi zaidi ya wavuvi wadogo wadogo Zanzibar ili kuleta maisha bora zaidi kwa zasficu katika nyanza zote za shughuli zao.