Na,Nishan khamis.
Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Balozi wa Itali aliyopo nchini Tanzania Giuseppe Coppola leo amefika katika kijiji cha Nungwi kwa niaba ya rais wa Itali katika hafla ya kumkabidhi tuzo ya mwanamke bora anaye saidia jamiii masikini katika nyanza zote ambaye ni mkurungezi wa taasisi ya Sister Island bi Francesca Michel aliyopo shehia ya kiungani Nungwi wilaya ya kaskazini A Unguja.
Balozi amesema bi Francesca amekuwa mwanamke anaye jitoa katika kuisadia jamaniii hasa masikini hali iliyopelekea rais wao kumpa tuzo ya mwanamke bora kutokana na mchango wake mkubwa wa maendeleo katika nchi mbali mbali Duniani.
Aidha amesema serikali ya Itali na Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano mzuri katika nyanza zote zikiwemo za kiuchumi, kisiasa, kijamii na uchumi kwa msingi ya kuimarisha maendeleo na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.
Pia amesema amevutiwa na ukarimu,utamaduni wa kizanzibar na jambo amabalo amefurahishwa kuona utulivu na utependo uliopo ni ishara ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika nyanza zote kwa maslahi ya kidemokrasia, kiuchumi na kijamiii kwa pamoja.
Mkurungezi wa Sister Island Francesca amesema amemshukuru rais wake wa Itali kwa tuzo iyo ambayo imekuwa ni chachu kwake kwa kuendeleza zaidi katika kuwasaidia wanajamii masikini na kuendelea kusaidia serikali katika utatuzi wa changamoto mbali mbali za wanajamii vinazo wakabili hapa Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Ametoa wito kwa jamiii hasa wazazi kuwa karibu katika kuwafatilia watoto wao kuhusu elimu ili kushirikiana kwa pamoja katika kuwaandalia mazingira rafiki ya kielimu ili watimize malengo yao kwa maslahi ya familia na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika Hafla iyo mhasibu mkuu wa taasisi hiyo ndugu,Haji Mohommed Ali amesema taasisi hiyo inajihusisha katika masuala ya elimu,afya,utamaduni masuala ya jamiii na michezo ambopo mpaka sasa imejenga skuli mbili nasari na msingi,imejenga visima 10 vya maji,gari za ambulance ileta mbili,vifaa vya tiba kama vile vitanda,viti,nguo viti vya operation imejenga uwanja wa michezo kwa watoto, utoaji wa mavazi na vyakula katika wanajamii wa mkoa wa kaskazini na Zanzibar kwa ujumla wamekuwa na desturi hiyo ya kuwasaidia wanajamii.
Msaidi wa sheha shihiya ya kiungani akizungumza kwa niaba ya sheha amesema ujio wa Balozi utafungua zaidi utalii katika kijiji cha Nungwi na zanzibar kwa ujumla jambo amabalo litazidi kuvutia watalii nchini na kuongeza zaidi pato la taifa.
Nao wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo wamesema wamefurahishwa na ujio wa balozi na kutoa pongezi za dhati kwa taasisi hiyo kwani imekuwa na mchango mkuwa wa kusaidia kutatua changamoto za jamiii kama vile maji, chakula nguo na uwepo wa skuli ya sister Island imesaidia kwa kiasi kikubwa wa
Wao kusoma vizuri kwa kaisi kidogo ukilinganisha na elimu bora na huduma wanazo patiwa katika skuli hiyo.
Hivyo waiomba serikali kuendelea kushirikiana ipasavyo na wawekezaji kam a hao katika kutatua changamoto na kuendelea kupeleka mbele maendeleo ya Nungwi na zanzibar kwa ujumla.

