Popular services

TAMASHA LA VIJANA ECO-FIT LAHIMIZA VIJANA KUTUNZA AFYA ZAO.


Na,Nishan khamis. 

Zanzibar. 

Taasisi ya ZAFAYCO kwa kushirikiana na MARIE STOPES TANZANIA leo wameendelea kufanya Tamasha la vijana eco-fit,Tamasha ambalo lilijumuisha michezo ya aina mbali mbali, utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana pamoja na jamii kupata nafasi ya kupima maradhi mbali mbali ambapo Tamasha hilo  limewakutanisha vijana wa mkoa wa kaskazini Unguja ambalo lilifanyika katika kiwanja cha mpira Mail nane wilaya ya Magharibi A Unguja. 

Mstahiki Meya baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini A Unguja Machano Fadhil Machano (Babla)ambaye  ni mgeni rasmi katika Tamasha hilo amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inathamini mchango mkubwa kutoka sekta binasfi juu ya kuwasaidia vijana katika katika nyanza zote kwa misingi ya ushiriano mzuri wa kupeleka mbele maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.

Mstahiki Meya amewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu pamoja na kutumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya nchini bali kuwa wazalendo na kushirikiana na serikali na taasisi binasfi katika kutatua changamoto zinazo wakabili kwa misingi ya maendeleo ya vijana nchini na taifa kwa ujumla. 

Aidha Babla amewapongeza Taasisi ya ZAFAYCO na MARIE STOPES TANZANIA kwa maandalizi mazuri yenye kuvutia na yenye taswira halisi ya kuwasaidia vijana katika katiak kuwainua kiuchumi pamoja na kuwapatia elimu sahihi ya kutunza afya zao ukizingatia vijana ndio taifa na sasa na lijalo.

Mratibu wa ZAFAYCO Mohamed Jamal awali akimkaribisha mgeni rasmi amesema taasisi hiyo ambayo siyo ya kiserikali inajushughulisha na changamoto mbali mbali za vijana nchini inaendelea kuwasaidia viijana katika katika nyanza mbali mbali za kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana,kuwawezesha vijana kiuchumi katika harakati zao za ujasirimali, utoaji wa elimu ya uraia ikiwa lengo ni kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa misingi ya kushirikiana na serikali kwa ukaribu kwa maendeleo ya vijana na taifa zima.

Denice Simeo afisa vijana Marie Stopes Tanzania amesema kwa kushirikiana na Zafayco kupitia mradi wa Startsmall wenye lengo la kutoa elimu ya huduma za afya za uzazi pamoja na ujasirimali kwa vijana ili kuwaepusha vijana na mimba za mapema zisizo tarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na kuwewezeaha kiuchumi vijana kwa misingi ya maendeleo ya vijana nchini. 

Denice amesema vijana ndio wahanga wakubwa wa mambo mbali mbali hivyo ametoa wito kwa vijana kuwa makini kulinda afya zao kwa kutumia vyanzo rasmi vya taarifa na huduma sahihi za afya za uzazi. 

Kwa upande wao vijana wamesema bado kuna tatizo la baadhi ya vijana wa vijijini kukosa elimu ya afya ya uzazi jambo linalo pelekea uwepo wa mimba zisizo taraijwa kwa vajana wa vijijini. 

Wamewapongeza waandaaji wa Tamasha hilo na elimu ya afya ya uzazi waliyoipata na kuwahidi kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao kwa misingi ya ujenzi wa afya bora kwa vijana nchini. 

Wadau toka serikalini, taasisi mbali mbali na makundi mbali mbali kutoka mkoa wa kaskazini waliohudhuria katika Tamasha hilo ikiwa ni mikakati ya kuendeleza harakati za utatuzi wa changamoto za vijana nchini kwa maslahi ya vijana na taifa zima.