Popular services

UDHALILISHAJI WA UTELEKEZAJI WA FAMILIA WACHUKUA SURA MPYA KASKAZINI UNGUJA.


Na,Nishan khamis. 

Mkoa wa kaskazini Unguja. 

Mkuu wa dawati la jinsia la wanawake na watoto  mkoa wa kaskazini unguja mahonda, Inspector Salum Khamis Machano amesema kwa sasa Kesi nyingi zinazo ripotiwa za udhalilishaji katika ofisi yake ni Kesi za udhalilishaji wa utekelezaji wa familia hali ambayo imechukua sura mpya kwa kasi ukilinganisha na hapo awali. 

Inspector Salum ameyasmea hayo leo huko kinyasini wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji katika mkoa huo.

Amesema familia nyingi zitatekelezwa hali ambayo inapelekea wanawake na watoto kudhalilika kutokana na kukosa mahitaji muhimu mbali.

Amesema kupitia siku 16 hizo amewaomba wanajamii mkoa huo kushirikiana na jeshi la polisi na wanaharakati mbali mbali katika kuodoa aina zote za udhalilishaji katika mkoa huo.


Akizungumza katika uzinduzi huo mkurungezi wa baraza la mji  wilaya ya kaskazini B Unguja Abdurahman Ali Mukhtar ametoa wito kwa wanaharakati na jamii kwa ujumla kuendelea kutoa elimu zaidi juu ya madhara ya matendo ya udhalilishaji ili kupunguza na kuondoa kabisa vitendo hivyo nchini huku akiwataka wananchi kuacha muhali na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na mahakamani wakati wa kutoa ushahidi ili kutokomeza vitendo hivyo. 

Naye mwenyekiti wa Juvikuka Asma Ali Makame amesema ipo haja kwa wanajamii kafanyia kazi elimu inayotolewa na wanaharakati wa kupambana na vitendo hivyo ili kuleta nguvu ya pamoja katika kutokomeza matendo hayo licha ya elimu kutolewa lakini bado vitendo hivyo vinaendelea hivyo kwa mshikanamo wa pamoja utaleta tija katika mapambano dhidi ya udhalilishaji mkoa huo.

Ametoa wito kwa wazazi kuwa na utamaduni wa kufuatilia nyendo za watoto wao na kuwa nao karibu ili kuwaepusha na hatari mbali mbali zinazo weza kuwafika.