Popular services

UZINDUZI WA KAMPENI MJUE JIRANI YAKO IDARA YA UHAMIAJI M/KUSINI UNGUJA.

 Na,Nishan khamis. 

Mkoa wa Kusini Unguja.

Wananchi mkoa wa Kusini Unguja wametakiwa kushirikiana na idara ya uhamiaji mkoa huo  katika kudhibiti vitendo vya uingiaji wa wahamiaji haramu nchini kwa misingi ya kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

Hayo ameyasema kamishina msaidizi afisa uhamiaji idara ya uhamiaji mkoa wa Kusini Unguja Tahir Khamis Mussa wakati akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya mjue jirani yako mkoa huo iliyofanyika katika ukumbi 

 wa skuli ya sekondari kizimkazi wilaya ya Kusini Unguja. 


Amesema uzinduzi wa kampeni hiyo lengo lake ni kuwapa elimu wananchi  kuwatambua wageni waliopo katika maeneno yanayo tuzungaka ili kuwabaini   wenye uhalali wa kuishi nchini na kuwatambua wasio kuwa halali kwa misingi ya kupambana na wahamiaji haramu nchini ambapo ametoa wito kwa jamiii kushirikiana na jeshi la uhamiaji katika mapokezi ya kamepeni hiyo kwa misingi ya kuimarisha ulinzi na usalama nchini.


Mkaguzi Msaidizi idara ya uhamiaji mkoa huo Muhsin Moh'd Haji na Mwajuma Makame Faki wakiwasilisha mada mbali mbali katika uzinduzi huo wamesema mtu anaweza kupoteza uraia endapo ikibainika urai huo ameupata kwa njia ya udanganyifu ambapo waziri mwenye zamana anaweza kumfuta mtu huyu uraia wa Tanzania kutokana na udanganyifu alioutenda jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kupitia kampeni hiyo wamewashauri jamii  zaidi kuwatambua wageni na majirani mbali mbali wananoingia nchini ili kudhibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo biashara haramu ya binadamu,uingiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya jambo ambalo ni kosa kisheria nichini Tanzania.

Aidha wametoa wito kwa wale wote wanao taka kwenda nchi za nje kufanya kazi ni vyma wakafuata utaratibu mzuri kupitia idara ya uhamiaji ili kuepukana na njia za udanganyifu hali amabyo ni kosa kisheria.

Mada nne ziliwasilishwa katika uzinduzi huo zikiwemo  uraia,taratibu za kufuata mgeni anapo taka kuingia nchini, muhamiaji harama na athari zake, mada juu ya passport pamoja na biashara haramu ya usaafirishaji wa binadamu jambo ambolo limekuwa likitokea nchini.

Isaya palijodai ni miongoni mwa washiriki waliopatiwa elimu hiyo katika uzinduzi amasema kwa upande wake elimu hiyo imemnufaisha vikubwa kwani alikwa hajui kuwa Tanzania haina uraia pacha pia amejivunia elimu ya uraia,namna ya utaratibu wa kupata passport pamoja na kuvujia madhara ya biashara haramu ya binadamu. 

"nimejifunza mengi katika ujio wa kamepeni hii kwani nilikuwa sijui maswla ya uraia,passport na bishara haramu sasahivi nimeelewa vizuri ninawapongeza idara ya uhamiaji kwa elimu hii"

Tatu Hassan Juma naye ni mnufaika wa elimu ya mjue jirani yako amesema amefarijika na elimu aliyoipata kwani amejifunza mengi ambayo alikuwa hayajui hivyo ametoa shukrani za dhati kwa jeshi la uhamiaji huku akiahidi kuwa Balozi kwa wengine kuwapatia elimu hiyo kwa misingi ya ushiriaano wa pamoja na idara na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuendeleza kuimarisha usalama na amani nchni.