Popular services

ACT- WAHIMIZA WANAWAKE KUZIKIMBILIA FURSA ZA UONGOZI.

FAKI MBARAKA NA NISHAN KHAMIS. 

Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Taifa Mhe. Othmani Masoud Othmani amewataka wanawaweke nchini kuwa mstari wa mbele kupigania mabadiliko ya kiuchumi katika nchi Yao ili kuimarisha ustawi WA jamii.

Mhe. Othmani ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la ngome ya Wanawaweke wa Chama hicho lililofanyika katika ukumbi wa majidi holi Kiembe samaki.

Amesema Hali duni ya kiuchumi iliyopo nchini waathirika wakubwa ni wanawaweke kutokana na kupata wakati mgumu wakati wa malezi ya familia na huduma muhimu  za watoto.

Mhe. Othmani  Ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Hata hivyo amewahimiza wanawaweke nchini kua mstari wa mbele kusimamia haki na kupinga dhulma na ufisadi  ili kuimarisha utawala wa Sheria pamoja na ukuaji wa uchumi katika nchi Yao.

Mapema Makamo Mwenyekiti wa ngome ya Wanawaweke wa Chama hicho Bi Umra hamadi Sadala amewataka wanawake kuwa kipaumbele katika kuzikimbilia fursa za uongozi pindi wakati ukifika pia amewaomba wanawaweke nchini kuunga mkono Chama hicho ili kupigania masilahi ya Taifa lao.

Katika Kongamano Hilo Jumla ya mada mbili zimejadiliwa ikiwemo wanawake na uongozi pamoja na mwanamke jasiri huku likibeba kauli mbiu ya "Wanawaweke na ushindi 2025".


Kupitia  kongamano hilo  wanaharakati wametoa wito kwa vijana hususani wanawake wasimame imara na kuhakikisha wanapeleka mbele maendeleo ya chama na kufikia azama ya chama hicho.