Na,Nishan khamis-Zanzibar.
Imeelezwa kuwa uwepo wa amani na utulivyo na uimarishawaji wa miundombinu nchini ni kigezo kikubwa cha kuongeza uingiaji wa watalii nchini hali inayopelekea kutoa fursa za kujiajiri vijana na wanawake na Kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya utalii nchini.
Hayo ameyasema leo mtafiti Clemence Abex Msingwa kutoka taasisi ya Inspire Consultants katika ukumbi wa ZSSF kariakoo wakati akizungumza na wadau mbali mbali wa utalii, taasisi mbali mbali za vijana na baadhi ya wajumbe toka serikalini katika kuangazia utafiti na Inspire Consultants uliodhaminiwa na shirika la actionaid Tanzania katika kuanagalia juu ya ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta ya utalii nchini.
Clemence amesema Ujenzi wa miundombinu ya barabara ,amani na usalama pamoja na fukwe nzuri za kuvutia ni mambo yanayo ongeza idadi ya watilii kutoka 260,644 hadi 638,498 mwaka 2023 inatokana na jitihada kubwa za serikali katika kuimarisha miundombinu mizuri hali inayopelekea kuwavutia watalii kuja nchini na kutoa fursa kwa vijana na wanawake katika kujikwamua kiuchumi.
Amesema katika utafiti huo uliodhaminiwa na actionaid Tanzania ulifanyika katika mkoa wa kaskazini Unguja ambapo watu mia mbili walihojiwa kati yao Wanawake 108 na wanaume 92 ambapo utafiti ulibaini kuwa ukosefu wa vigezo watu kwa wanawake katika utalii,mawazo potofu juu ya utalii ni uhuni ni changamoto kwa wanawake kushiriki ipasavyo katika utalii nchini.
Hivyo amewahimiza wazazi kuwapa nafasi vijana wako katika kutimiza malengo yao katika utalii pamoja na wanawake kuzikimbilia fursa zilizopo katika utalii ili wajiajiri na kuweza kujikwamua kiuchumi kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Mratibu wa actionaid Zanzibar Bakar Khamis amesema kutoka na changamoto mbali mbali za kitalii kwa vijana na wanawake mkoa huo waliamua kuwapa tenda Inspire Consultants kufanya utafiti na kujua changamoto ili kupata ufumbuzi na vijana na wanawake kuweza kuziona fursa za kitalii ilia kuzikimbilia kwa misingi ya kujiajiri na kuweza kupata kipato kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Bakar amesema actiaid inaendelea na program zake katika kuwasaidia wanajamii kuziona fursa kwa misingi ya kupunguza changamoto za ajira nchini.
Ametoa wito kwa vijana na wanawake ikiwa utalii unachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa na kutokana na utafiti huo ni vyema kuzikimbilia fursa za kitalii zilizopo nchini.
Baadhi ya washiriki katika kikao hicho wamesema baadhi ya wazazi wana dhana potofu juu ya maswala ya utalii lakini kupitia Halal Tourism imetoa mwangaza kwa jamiii kuona kuwa utalii si uhuni, bali jamii iendelee kuunga mkono juhudi za kimaendeleo katika zinazo fanywa nchini ili kuwavutia watalii kwa maendeleo ya taifa.
Wameshauriwa vijana na wanawake kuchangamkia fursa za utalii nchini kwa lengo la kujiajiri kwa misingi ya uimarishaji wa maendeleo ya jamiii na taifa kwa ujumla.