Na,Nishan khamis.
Wilaya ya Kati Unguja.
Jumuiya ya vijana ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji mkoa wa kaskazini Unguja(JUVIKUKA) imelaani kitendo cha udhalilishaji na kuuwawa mtoto wa miaka sita tukio lilotokea Alhamis 14 Novemba 2024 katika shehia ya ubago wilaya ya kati Unguja.
Hayo ameyasema leo mkurungezi wa JUVIKUKA Asma Ali Makame walipo mtembelea na kumfaji mama wa mtoto na familia kwa ujumla kutokana na mtihani ulio wakuta.
Ameseme wanalaini vikali kitendo hicho na vitendo vyote vya udhalilishaji vinavyo tendeka nchini, hivyo wameiomba serikali kufanya jitihada zaidi kumkamata aliye tenda kosa hilo na hatua zaidi za kisheria zichukuliwe ili kutokomeza vitendo hivyo nchini.
Akizungumza kwa niaba ya familia Amina Said Moh'd ambaye ni mama mdogo wa marehemu amesema wamehuzunishwa kwa kiasi kikubwa kutoka na kitendo cha kikatili dhidi ya mtoto wao na wameimba serikali kuchukua hatua stahiki kwa watendaji wa kitendo hicho cha kikatili.
Hata hivyo wameishukuru serikali,juvikuka,wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kwa ukaribu wao wa kuwafariji na kuwapa moyo wa subra katika kipindi kigumu walicho nacho.
Naibu sheha wa Ubago Juma Pandu Mtwana amesema kwa kushirikiana na serikali wanaendelea kumtafuta mtendaji wa kosa hilo na ameiomba jamii ishirikiane katika kuwafichua wahalifu wa vitendo viovu katika shehia iyo.
Abdi Ame Makame kijana kutoka juvikuka amesema jumuiya yao imehudhunishswa na kitendo hicho ivyo wanaungana na serikali na wadau mbali mbali katika kupambana na vitendo hivyo nchini.
Aidha ametoa wito kwa mama mtoto na familia kuwa na subra katika kipindi kigumu bali kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote.
Nao baadhi ya majirani wamesema wamehuzunishwa na tukio hilo hivyo wameahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi na wadau mbali mbali katika kuwatafuta watendaji wa kosa hilo kwa misingi ya kutokomeza vitendo hivyo nchini.