Na,Nishan khamis.
Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Wazazi na walezi wadi ya kilimani tazari jimbo la Nungwi wilaya ya kaskazini A Unguja wamehimizwa kuwapeleka skuli watoto wenye ulemavu pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu wa skuli ya maandalizi kilimani ili kuwajenga watoto kusoma kwa bidii kwa maslahi ya familia na taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema leo mstahiki Meya baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini A Unguja Machano Fadhil Machano (Babla) ambaye ni mgeni rasmi katika Mahafali ya pili skuli ya maandalizi kilimani Tazari.
Amesema watoto wenye ulemavu wana haki sawa kama watoto wengine hivyo wanawajibu wa kuwapeleka skuli na kutoa ushirikiano baina ya wazazi na walimu ni jambo la misingi katika kujenga misingi mizuri ya elimu kwa watoto kwani ukosefu wa mashirikiano ya wazazi, au walezi na walimu inaweza kupeleka watoto wakakosa haki yao msingi katika upatikanaji wa elimu bora.
Kupitia risala ya mahafali hiyo mgeni rasmi amewahimiza wazazi kuwa karibu na walimu,kamati za skuli na vikao vya mara kwa mara ikiwa ndio njia ya kutatua changamoto mbali mbali na kuweka mikakati imara ya kuwapatia elimu bora watoto kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Awali Diwani wadi ya kilimani tazari Talib Haji Abas akimkaribisha mgeni rasmi amesema ameishukuru serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kuimarisha miundoni ya elimu katika wadi hiyo, ivyo amewtaka wazazi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo pamoja na kushirikiana na walimu katika kuleta mafanikio ya elimu ngazi zote katika wadi na jimbo kwa ujumla.
Mwalimu mkuu skuli ya maandalizi kilimani Fatma Wadi Ame asema miongoni mwa changamoto zinazo wakabili ni ukosefu wa computer na mashine ya kutolea photocopy ni jambo linalo wapa wakati mgumu kutofanikiwa baadhi ya majukumu yao.
Kwa uapnde wao wanafunzi wakisoma risala katika shuguli hiyo wameeleza kuwa baadhi ya wazazi kukosa kutoa ushirikiano kwa walimu ni jambo linalo rejeaha nyuma maendeleo kwa baadhi ya watoto katika skuli hiyo.
Nao baadhi ya wazazi wamesema watahakikisha wanawahasisha wazazi wenzao katika kutoa ushirikiano mkubwa kwa walimu ikiwa ni wajibu wao kwa maendeleo ya watoto wao,familia na taifa kwa ujumla..
Jumla ya wanafunzi ya wanafunzi 158 wamehitimu elimu ya maandalizi wakiwa wanaume 77 na wanawake 81 wakijiandaa kuingia elimu ya msingi mwaka 2025.