Na,Nishan khamis.
Wilaya ya kaskazini A Unguja.
Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya kaskazini A Unguja (NAPAC) imesema aslimia 65 ya wanawake wilaya hiyo wanakabiliwa na matatizo ya kisheria
Hayo ameyasema afisa ufuatiliaji na tathmini wa NAPAC Khamis Kombo Ali hapo jana wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya ripoti ya majumuisho ya ziara ya utoaji wa msaada wa kisheria (legal aid clinic) katika shehia ya Chaani Kikobweni, Kivunge na Tumbatu Gomani.
Amesema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto mbali mbali za wanajamii na mtu mmoja mmoja ambapo jumla ya wanajamii 362 wameshiriki katika shehia hizo tatu ,wanawake wakiwa 260 na wanaume 102.
Katika ziara hiyo wasaidizi wa sheria walitoa msaada wa kisheria kwa wanajamii 75 wanawake wakiwa 49 na wanaume 26 ambapo mashauari yaliyo sikilizwa yanahusu malezi ya watoto ni mashauri 26,ardhi 6,ndoa 4,utekelezaji 6 na haki za kiraia 33.
Afisa amesema matokeo yameonesha kwamba ukosefu wa malezi ya pamoja,umasikini, ukosefu wa elimu ya kiraia ndio chanzo cha matatizo katika jamii.
Pia matokea yanaonesha wanawake ndio wahanga wakubwa wa matatizo ya kisheria ni sawa na wastani wa asilimia 65 ya kesi zilizopatiwa msaada wa kisheria.
Watu 57 walipatiwa ushauri wa kisheria, mashauri 8 yalipatiwa rufaa(dawati la jinsia Mahonda) na mashauri 10 yapo katika hatua ya ufuatiliaji wa maeneo tofauti kupitia NAPAC.
mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa kaskazini Unguja Inspector Salum Khamis Machano amesema amesema kwa kesi za utekelezaji ndizo zinazo ripotiwa zaidi katika dawati hilo.
Hivyo amesema jamiii inahitaji elimu kusuhu malezi ya kujitambua na haki za binadamu ili ipate uelewa wa kuweza kujua hazi zao kuwa na utashi wa kufuatilia haki zao.