Na,Khamis Nishan.
Zanzibar: Katika jamii inayokua kwa kasi, suala la rasilimali watu lina nafasi kubwa katika uongozi hasa kwa wanawake,umuhimu zaidi katika kuwainua wanawake kuwa viongozi katika nyanza zote nchini. Hadia Ali Makame mwanamke aliyepambana na kuwa kiongozi katika vikundi na jumuiya katika kuleta mabadiliko ya wanawake wenzake Mkoa wa Kaskazini Unguja.Alizaliwa miaka 58 iliyopita,katika Kijiji cha Chaani Masingini Wilaya ya Kaskazini A,Unguja Mkoa wa Kaskazini Unguja amekulia katika Kijiji cha Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A Unguja Mkoa wa kaskaziniUnguja,aliolewa mwaka 1986 bila ridhaa yake na kufanikiwa kupata watoto tisa lakini kwa sasa ana watoto saba baada ya watoto wawili kufariki watoto wakike watato na wakiume wawili.
Tangu usichana wake Hadia amekuwa mwanaharakati wa kupambana changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mwkaa 1984 -1986 alijiunga na kikosi maalum cha kujitolea (KMCK) kwa sasa ni kikosi cha Valentia Zanzibar (KVZ) , mwaka 1990 alianza ushawishi kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini na kuanzisha kikundi cha Rabbi Tuongoze Mkokotoni yeye akiwa katibu wa kikundi."Nimefanya mengi ya ushawishi wa maendeleo kwa wanawake na vijana katika mkoa wangu na nje ya mkoa nikiwa na malengo ya kuhamasisha wanawake kujikwamua kiuchumi,kupiga vita vitendo vya udhalilishaji pamoja na kuzikimbilia nafasi za uongozi katika nyanza zote kwani mkoa wetu wanawake tulikuwa tumelala ila sasa wapo vizuri". Amesema Hadia ambaye pia alianza ujasirimali mwaka 1999 alipojiunga na Jumuiya ya Kuhifadhi Mazingira Mkokotoni.
Hadia aliendelea na ushawishi wake wa kimaendeleo ambapo mwaka 2000 alifanya ushawishi na kuanzisha Nasari ya Madrasat Najat Mkokotoni na imekuwa na msaada mkubwa kwa wanajamii ‘’nimefanya mengi ya ushawishi wa maendeleo kwa wanawake na vijana nikiwa na malengo ya kuwashawishi katika kujikwamua kuichumi,kupiga vita vitendo vya udhalilishaji pamoja na kuwahamsisha kuzikimbilia nafasi za uongozi katika nyanza zote kwani wanawake tulikuwa tumelala ila kwa sasa alhamdullah’’Amesema Hadia.
Mariam ni mtoto wa nne katika familia ya Hadia amesema tangu akiwa mtoto amemshuhudia mama yake akiwa na pirika mbalimbali za uchechemuzi wa maendeleo ya wanawake na vijana ”Hakuna siku anayo tulia watu wengi hufika nyumbani mara kwa mara anashiriki semina ambazo zimemjenga katika harakati zake licha ya kuwa baadhi ya watu hawapendi maendeleo ya mama lakini sisi tuna muunga mkono kwa asilimia zote hata mimi sasa hivi nafuata nyao zake " Amesema Mariam ambaye anajivunia uthubutu wa mama yake.
Katiba ya Tanzania inatoa fursa sawa ya ushiriki wa wanawake na wanaume katika nyanja zote za maisha, sura ya 3 Ibara ya 12(2) inatoa haki ya kuheshimiwa.Tamko la kimataifa la haki za binadamu pia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inasisitiza usawa wa kijinsia.
Mohamed Abdalla Ali ni jirani wa Hadia kwa muda wa miaka 28,amesema wakati wowote tunapokuwa na changamoto hapa mtaani amekuwa na msaada mkubwa katika kutusaidia maswala ya kisheria kutuhamasisha katika maendeleo na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji.”Harakati za maendeleo hususan masuala ya vijana na wanawake amekuwa mstari wa mbele sana kwetu hata mimi binafsi nilipatwa na matatizo lakini alinisaidia kwa kiasi kikubwa" Amesema Mohamed ambaye anaona uongozi kwa wanawake ni maendeleo ya jamii.
Baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari, Hadia alipata fursa ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) mwaka 2007 aliposomea kozi ya Stashahada ya uwalimu wa msingi ambapo hakuendelea kutokana na sababu za kimaisha zilizo mkabili. Mwaka 2012.Hadia alifiwa na mume wake akiwa katika masomo ya usaidizi wa sheria mwaka wa kwanza ilimdhohofisha kimasomo. “Kipindi alichofariki mume wangu nilifikwa na majozi makubwa ambayo yalidumu kwa muda mrefu huku nikiwaza jinsi ya kuwalea wanangu na ilipeleka kukata masomo mwaka mmoja kutokana na msongo wa mawazo baadae nikarudi katika hali yangu ya kawaida na kuendelea na harakati zangu ” Amesema Hadia ambaye huku akiwa na huzuni.
Licha ya harakati zake Hadia anajishughulisha na ukulima,amekuwa mstari wa mbele kwa mtandao wa wakulima wadogowadogo kisiwani hapa,Septemba 2024 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa mtandao wa wakulima wadogowadogo –MVIWATA Zanzibar na sasa anaendelea na harakati zake akiwa na vikundi na taasisi mbalimbali katika shughuli zake." Nilishawishiwa na TAMWA-ZNZ na watu wengine nigombee Ubunge na niligombea ila sikuwa na wajumbe wa kutosha ila nilipata kura na kupata nafasi ya tatu pia nina,Tuzo mbalimbali za mpambanaji bora wa kupinga vitendo vya ukatili Zanzibar"Amesimulia Hadia.
Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ),Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya mazingira,jinsia na utetezi Pemba (PEGAO) mwaka 2020-2023 walitekeleza mradi wa kuwawezesha wanawake na jamii kudai haki zao za kidemokrasia na uongozi ambapo wanawake 200 kupitia mradi huo waliwezeshwa na kujengewa uwezo kuhusu masuala ya ya kidemokrasia, siasa na uongozi ili waweze kushiriki katika vyombo vya maamuzi.Asia Fadhil Makame,Mkurungezi wa Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Kaskazini A Unguja –NAPAC amesema ,“Tangu mwaka 1984 namfahamu vizuri katika utendaji wake wa uhamasishaji na kupambania maendeleo ya wanawake na vijana amekuwa mstari wa mbele hata huu ukurugenzi wangu amenitia moyo sana mpaka kufika hapa”. Amesema Asia huku akiona kuwa harakati za Hadia zimemvutia na jinsi jamii inavyomuamini. “Hali hii imenipelekea na mimi kuvaa viatu vyake mpaka mwaka 2023 nimepata Tuzo ya mwanamke bora kwa kufanya uchechemuzi wa wanawake katika vikoba hii yote ni hamasa na kujifunza kwa mama yetu Hadia "Amemaliza Asia.
Kwa bidii na maono yake makubwa, Hadia amejidhihirisha kuwa mwanamke ambaye ameweza kuleta mabadiliko na kuwa kiongozi kutokana na rasilimali watu” kwa kweli nazivunia kuendelea kuwapambania vijana na wanawake wenzangu katika changamoto za kisheria pamoja na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji nitaendelea na msimamo wangu wa mabadiliko ya wanawake “ Amemalizia Hadia.
