Ofisi ya mkuu wa wilaya ya kaskazini A Unguja imetoa tamkoa la kupimwa vipimo vya maradhi ya malaria kwa wafanyakazi wa sehemu za ujenzi, wafanya biashara mama ntilie pamoja na vituo vyote vya boda boda katika kijiji cha Nungwi.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya kwa Afisa Mipango wilaya hiyo Abdulmajid Dhamir Ramadhan wakati akizungumza na wamiliki,wasimamizi wa hotel za Nungwi, wafanya biashara wa mama lishe,boda boda ,maafisa wa kitengo cha malaria pamoja na maafisa mbali mbali katika wilaya hiyo.
Amesema kutoka na hali ya uwepo wa ugonjwa huo katika wilaya hasa maeneno ya Nungwi serikali ya wilaya imewataka wasimamizi wa ujenzi, wamiliki wa hoteli,walinzi,waendesha boda boda na wajasiriamali kwa ujumla maneno ya Nungwi kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wa muda na wale wa kudumu wanawajibika kupima vipimo vya malaria kabla ya kufanya kazi katika vituo vya afya vilivyo sajiliwa na kupatiwa vyeti vya uthibitisho wa Daktari ikiwa ni mipango ya mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo eneo hilo na wilaya kwa ujumla.
Amesema kuwa hatua hiyo ni lazima na itafuatiliwa kwa ukaribu zaidi ikiwa lengo ni kudhibiti maradhia hayo na Amesisitiza endapo mtu yoyote akikiuka agzio hilo kanuni na sheria zitachukua mkondo wake.
Kwa upande wake Meneja wa program ya kumaliza malaria Zanzibar Dkt Shija Joseph Shija amesema hali ya ugonjwa huo kwa miaka miwili iliyopita hali ilikwa si nzuri maambukizi yalikuwa makubwa nchini lakini mwaka 2025 hali imepungua licha ya kuwa wilaya ya kaskazini A Unguja hivi sasa inaongoza kwa maambukizi hayo ukilinganisha na miaka miwili ya nyuma.
Amebainisha kuwa tatizo la wilaya hiyo kuwa kinara hivi sasa katika maradhi hayo hasa eneo la Nungwi linatokana na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka sehemu mbali mbali na sehemu hatarishi zaidi ni sehemu za ujenzi,sehemu za biashara ,wajasiriamali na waendasha boda boda na waathirika zaidi ni vijana kauanzia rika la miaka 15 hadi 35 asilimia 70 ya vijana wa kiume ndio waathirika wakubwa wa maradhi hayo.
Hivyo amesema njia ya kudhibiti tatizo hilo ni kutumia vyandarua,dawa za kujikinga na mbu,kuvaa nguo refu hasa wakati wa usiku,kuangalia afya mara kwa mara na kushirikiana timu ya afya wilaya hiyo katika kudhibiti tatizo hilo.
Nae,Afisa mtambuka wa programu ya kumaliza malaria Zanzibar Safia Mohammed amesema kutoka na tatizo hilo kuwa kuwa eneo hilo ni lazima sasa sheria ya afya ya jamii iliyosainiwa mwaka 2017 itumike kwani katika sheria hiyo kuna kanuni ya kumaliza malaria na endapo akitokea mtu akisababisha maradhi hayo au akikataa basi faini yake ni shilingi laki tano au kifungo cha miezi mitatu au adhabu zote kwa pamoja.
Akitilia mkaza wa kwa wananchi dhidi ya kudhibiti tatizo hilo Daktari zamana wa wilaya hiyo Himid Juma Khamis amesema timu ya afya ya wilaya itahakikisha inafika maeneo husika ili kutekeleza majukumu yao kwa njia ya kudhibiti tatizo hilo hivyo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano mkubwa ili kutokomeza maradhia hayo na kuifanya wilaya hiyo kuendana na kauli mbiu ya kuwa na malaria zero nchini.
