WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA MALENGO ILI WAFIKIE NDOTO ZAO.
Mjumbe wa kamati ya siasa jimbo la Tumbatu Shadya Haji Omar amewahimiza wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Jongowe kusoma kwa malengo kwani kutawasadia kuwa wafanisi na kuweza kufikia malengo yao katika maisha.
Shadya ameyasema hayo hapo jana alipo alikwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kambi ya Wanafunizi wa kidato cha nne skuli ya sekondari Jongowe ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2023.
Hata hivyo Shadya amewataka wanafunzi hao kushirikiana,kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa wazazi na walimu kuhakikisha wanakuja kufanya vyema katika mitihani na kuendelea na elimu zingine ili kuendana na kasi ya elimu na ajira kwa hivi sasa Duniani na kuwa msaada kwanye familia na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mwalimu mkuu ndugu Bakar Ali Juma amesema licha ya jitihada kubwa walizo chukua kwa kushirikiana na kamati skuli pamoja na wazazi juu ya kuandaa maandalizi ya kambi iyo na amemuomba mgeni rasmi kuendelea kuwa naye katika kipindi hichi na kijacho katika kupeleka mbele maendeleo ya elimu katika skuli hiyo.
Akitoa nasaa zake kwa niaba ya wazazi wenzake Mzee Ali Khamis Shehe amewanasihii wanafunzi kusikiliza na kuzingatia yale yote wanayo fundishwa na kusoma kwa bidii na mashirikiano zaidi ili iwe shabaha nzuri ya mafanikio katika mitihani yao ya Taifa.
Wakitoa shukrn za dhati katika hafla hiyo mwanafuzni Ali Omar Ali na Twuwaiba Seleman Ali kwa niaba ya wanafunzi wenzao wamesema wameshukuru kwa nasaha za mgeni rasmi, wazazi na walimu walizo zitoa na watahakikisha wanazifanyia kazi na kuleta ufaulu mzuri katika skuli hiyo.
Na, Nishan khamis
