MBUNGE NA MWAKILISHI WACHANGIA MILIONI 12,800,000 KWA WANAFUNZI WA KAMBI.
NA,NISHAN KHAMIS.
Mbunge na mwakilishi wakabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 12,800,000 kwa wanafunzi wa msingi na sekondari jimbo la Tumbatu.
Mbunge Juma othman na mwakilishi Haji Omar Kher jimbo la Tumbatu jana walikabidi vyakula vya aina mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 12,800,000 na kwa ajili ya kuwachangia wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari jimbo la tumbatu wanao jianda na mitihani ya taifa inayo tarajiwa kuanzi hivi karibuni.
Akizungumza na wazazi,walimu na wanafunzi kwa nyakati tofauti Mbunge wa jimbo la Tumbatu Mhe Juma Othman amesema wamekuwa na utaratibu huo kwa kila mwka kuwachangua wanafunzi wa skuli jimbo hilo ili waweze kutulia na kujindaa vizuri kimwili na kiakili ili wafanye vyema.
Akizungumza kwa niaba ya Mhe, mwakilishi mjumbe wa kamati ya siasa jimbo la Tumbatu ndugu,Shadya Haji Omar amesema lengo la ziara ni kuwasaidia wanafunzi kwa kuwapa vyakula vya aina mbali mbali, utoaji wa vyeti na fedha taslim kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vizuri 2022-2023, ili kuwapa moyo na hamasa kwa wanafunzi wanao jiandaa na mitihani ya taifa.
Aidha ndugu Shadya amezitaka kamati za wazazi za maskulini na walimu kuvitunza na kuvitumia vyakula hivyo kwa lengo lililo kusudiwa ili viwasaidie wanafunzi katika kipindi chote wakiwepo kambini,na amewanasihii wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo na ndoto zao katika maisha.
Nao Wazazi na walimu kwa nyakati tofauti wamewapongeza viongozi hao kwa ukaribu wao wa kupeleka mbele maendeleo ya jimbo hilo.
Wakitoa neo la skukran wanafunzi Khuzaima Ali Habibu na Zuber Khamisi kutoka skuli ya sekondari ya Pale wamesema msaada huo utakuwa ni chachu kwao kujiandaa vyema kiakili na kimwili zaidi katika kipindi hichi na wamsema wanatarajia kufanya vyema kwenye mitihani yao inayo tarajiwa kuanzi hivi karibuni.
