MAJI YA ZAWA CHANGAMOTO KWA WAAKAZI WA MOGA NA CHUTAMA.
Na, Nishan khamis
Wakaazi wa shehia za Chutama na Moga wilaya ya kaskazin A wamesema ni kipindi kirefu wamekosa hudama ya maji ya zawa hali inayopelekea usumbufu mkubwa katika shughuli zao.
Kero hiyo wameitoa hapo jana katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na mkuu wa mkoa kaskazin unguja Mheshimiwa Ayoub Mohommed Mahmoud katika kusikiliza kero na Changaomoto shehia zote kwenye mkoa huo.
Amina kher Juma na Fatma Juma Rashid wakaazi wa shehi hizo wamemuomba mkuu wa mkoa kulishugulikia tatizo hilo.
Akijibu changamoto hiyo kwa njia ya simu kwenye mkutano huo afisa wa Maji wilaya ya kaskazini A Rashid Kasim Juma amekiri kuwepo tatizo hilo kwenye shehia hizo na amesema hivi sasa wanamalizia kutatua changamoto kama hiyo kwenye maoneno mengine na muda mfundi wanategemea kujenga tangi kubwa la maji kiashange na kuchimba kisima cha maji shehi ya chutama ili kutatua tatizo la maji maeneo hayo.
Mkuu wa mkoa amemtaka afisa huyo kulishugulikia tatizo hilo haraka iwezekanavyo ili wananchi wasipate tabu katika suala la maji kwenye mkoa huo.
Na, Nishan khamis.