Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe, Ayoub Mohommed Mahmoud anatarajia kufanha ziara katika shehia zote 75 za mkoa wa kaskazini Unguja.
Mheshimiwa Ayoub ameyasema hayo leo huko ofisini kwake mkokotoni wilaya ya kaskazin A alipokuwa akizungumza na masheha na makatibu wa masheha juu ya ziara yake katika mkoa huo.
Amesema huo ni utaratibu katika majukumu yake na lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ya shehi,kuimarisha mahusiano mazuri katika utendaji,kuongeza ufanisi wa uwajibikaji na kutatua kero na changaomoto zilizopo katika shehia husika.
Aidha Mhe, Ayoub amesema ziara iyo inatarajiwa kuanza tarehe 16 Agosti 2023 akiambatana na watendaji wa sekta mbali mbali ili waweze kutoa majibu,ufafanuzi na utambuzi wa papo kwa papo za changamoto zilizopo kwa wanajamii wa kaskazini.
Samba mba na hayo Mhe, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili katika shehi zao ili kuimarisha maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao masheha na makatibu wamemuhidi mkuu wa mkoa kuonesha ushirikiano kwa asilimia zote pindi ziara hiyo itakapo anza ikiwa ni mikakati madhubuti ya kuimarisha mahusiano na kuongeza ufanisi zaidi katika majukumu yao.
Na, Nishan khamis
