WAKAAZI WA KASKAZINI UNGUJA WATOA KAULI KUHUSU MWENDO KASI GARI ZA MCHANGA CHANZO CHA ONGEZEKO LA VIFO.
Na,Nishan khamis.
Wakaazi wa shehia za Potoa,muwange na pitanazako zilizopo wilaya ya kaskazin A Unguja wamesema madereva wa gari za mchanga wamekuwa wakisababisha vifo na ongezeko la watu wenye ulemavu kutokana na mwendo kasi wa gari wanazo endesha pasi na kufuata taratibu na kanuni za barabara.
Hayo wameyasema hapo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha skuli ya potoa ikiwa ni mwendelezo wa ziara za mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe,Ayoub Mohommed katika kusikiliza kero na Changaomoto za waakazi wa shehia mbali mbali mkoa huo.
Aidha wananchi hao wameimba serikali kuweka matuta katika eneo barabara ya skuli ya Potoa sehemu hiyo wanafunzi wanatumia wakinavuka wakienda skuli,kwani eno hilo limekuwa zikitokea ajali za mara kwa mara.
"Tunakuomba Mhe Ayoub utuekee matuta hapa maana hawa watu watatumaliza kwa jinsi wanavyo endesha gari zao kwa kasi kama mtashindwa hili sisi tunaweza ingili kati tukaweka magogo njiani maana tumechoka na hapa watoto wetu wanavuka wakienda skuli na sisi ndio njia yetu kubwa kwaiyo Mhe Ayoub tunaomba ulishughulikie hili" walisema wananchi.
Mhe Ayoub alieleza kwa kusikitishwa na baadhi ya madereva wanao kiuka sheria za barabarani na kumuagiza RPC kulishughulikia tatizo hilo mara moja .
Nae Kamishina msaidizi jeshi la polisi mkoa wa kaskazini ungua ndugu Daniel Emanuel Shila amekiri kuwepo kwa baadhi ya madereva wanao kiuka sheria na kanuni za barabara, amesema jeshi la polisi mkoa huo linaendelea na operation kali ya kudhibiti ukiukwaji wa sheria za barabara ili kupunguza ajali za barabarani mkoa huo.
Aidha Kamishina Shila aliwaeleza wanachi suala la matuta amelichukua kwa kushirkiana na mkuu wa mkoa na mamlaka husika kuona jinsi gani tatizo la uwekaji matuta sehemu iyo linafanyika haraka iwezekanavyo, amewataka wananchi kushirkiana na jeshi la polisi kuacha muhali kwa waarifu wa matukio hayo na mengine ili kuweza kutokomeza Matatizo hayo kwenye jamii.
