Popular services

RC, AYOUB AMEWASISITIZA MASHEHA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA UHAMIAJI KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU NCHINI

 


RC, AYOUB AMEWASISITIZA MASHEHA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA UHAMIAJI KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU NCHINI. 


Mkuu wa mkoa kaskazin unguja Mheshimiwa Ayoub Mohommed Mahmoud amewataka masheha kushirikiana ipasavyo na idara ya uhamiaji mkoa huo katika kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingia na wanao toka mkoa huo.


Mhe, Ayoub ambaye alikuwa mgeni rasmi jana katika kikao kazi kilicho fanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya idara ya uhamiaji mkoa wa kaskazini unguja na wakutanisha masheha wote wa wilaya ya kaskazini A pamoja na maafisa wa idara ya uhamiaji mkoa huo.


Mhe, Ayoub amesema mkoa wa kaskazini ni miongoni mwa mikoa inayoingiza wahamiaji wengi ni vyema masheha wakashirikiana ipasavyo na idara hiyi katika kuimarisha usalama na udhibiti wa wahamiaji haramu katika mkoa huo.



Hata hivyo RC Ayoub aliwataka masheha kutoa changamoto mbali mbali katika kikao hicho ili kujenga mikakati madhubuti ya kuimarisha ulizi na usalama kwa maendeleo ya mkoa na taifa ujumla.


Kamanda afisa wa idara ya uhamiaji mkoa wa kaskazini Unguja Tatu Burhan amesema idara ya uhamiaji mkoa huo ipo imara katika utekelezaji wa majukumu yao na awataka masheha na wananchi kushirkiana katika utoaji wa taarifa kwa wahamiaji harama ili kuendelea kulinda uslama na amani nchini.


Wakizungumza na mwandishi wa habar hizi sheha wa shehia ya matemwe kaskazini Wadi Ali Wadi na Bi Salama Khanis Juma sheha wa shehia ya chaani mcheza shauri wamesema kikao hicho kinatija sana kwa upande wao kwani kitawaongezea maarifa na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao.


Na,Nishan khamis