Popular services

RC AYOUB KUIMARISHA MICHEZO KASKAZINI UNGUJA.


 RC,AYOUB KUIMARISHA  MICHEZO KASKAZINI.

NA,NISHAN KHAMIS. 

Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe, Ayoub Mohommed Mahmoud amesema ameandaa bonanza kubwa kwa ajili ya kuhamasisha, kuimarisha na kuinaua  michezo kwenye mkoa huo.

Mhe, Ayoub ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Tumaini mkwajuni kwa kuzikutanisha shehia ya Kivunge, mkwajuni, kibeni na kidombo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mkoa huo. 

 Akijibu suala la ndugu Amour Simba kuhusu ni kwa namna gani ofisi ya mkoa imeandaa mikakati  ya kuinua vipaji vya mechezo kwnye mko huo, mkuu wa mkoa alieleza kuwa michezo ni fursa na ajira kwa vijana  hivyo ofisi yake imeenda mikakati madhubuti ya kulifanyia kazi sula hilo na hivi karibu wnatarajia kufanya bonanza kubwa litakalo shirikisha takribani timu 127, timu hizo zitapewa vifaa vya michezo ikiwa ni  harakati za kupeleka mbele sekta ya michezo kaskazini Unguja. 

Aidha RC Ayoub ametoa wito kwa wazazi,walezi na vijana na wadau mbali mbali katika kuliunga mkoa suala hilo na kuendela kujitokeza katika utoaji wa changamoto na kero kwenye ziara zake zinazoendelea mkoa huo ikiwa ni mikakati ya kupeleka mbele maendeleo ya kaskazin na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wao wakaazi wa shehia hizo  wamesema ikiwa michezo itapewa kipaumbele na ikapata wazamini itakuwa chachu kubwa ya kupunguza vitendo vya utumiaji wa madawa ya kulevya, uvutaji  bangi ,ulevi na itasaidia kupunguza vitendo vya uzalilisha kwenye mkoa huo.

"Unajua michezo inaodoa mawazo,fikra mbaya  na inajenga afya ambayo inamsaidia kijana kuweza kufikiri vitu vya msingi sasa matukio mengi yanayo tokea miongoni mwa tatizo sada ikiwa michezo itapewa kipaumbe inaweza kusaidia vijana wengi kuepukana na vitendo ivyo kwani sisi wa kaskazini kuna vipaji wakina fai toto wapo wengi uku tunamuomba Mhe Ayoub alizingatie hili".walisema vijana wa kaskazini. 


Na,Nishan khamis.