Popular services

WIZI WA MIFUGO NA MAZAO KERO KWA WAAKAZI WA MBALENI NA KITOPE


WIZI WA MIFUGO NA MAZAO KERO KWA WAAKAZI WA MBALENI NA KITOPE.

Na, Nishan khamis kaskazin unguja. 

Wakaazi wa Mbaleni na Kitope wilaya ya kaskazin B unguja,  wamesema wamekuwa wakisumbuliwa na vitendo vya wizi wa mifugo na mazao hali inayopelekea kuleta  ugumu wa maisha na  maendeleo katika maeneo yao.


Wameyasema hayo hapo jana katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika skuli ya Kitope wakitoa kero na changaomoto kwa mkuu wa mkoa kaskazin Unguja Mheshimiwa Ayoub Mohommed akiendelea na ziara zake za shehia kwa shehi kwenye mkoa huo.


Mati Khamis Kombo mkaazi wa Kitope amesema miongoni mwa sababu zinazo pelekea kuwepo tatizo hilo ni kukithiri  vijana wengi wakijihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na ulevi, hivyo amemuomba mkuu wa mkoa kulishugulikia tatizo hilo.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa ametoa onyo kwa wote wanao jihusisha  na vitendo hivyo waache mara moja kwani amendaaa mikakati madhubuti ya kutokomeza vitendo hivyo katika mkoa wake.


RC Ayoub amewataka Wazazi,walezi na jamii kuwapa taarifa hizo vijana wao kwani operation ikianza hakuna wakumuonea muhari atakaye kutwa na hatia ya vitendo hivyo.