Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya kaskazini A Unguja Rauhia Hassan Bakar amewataka wanafunzi kutambua matumizi sahihi ya mitandao ili iwasaidie katika masomo na kufikia malengo yao ya kielimu na maisha kwa ujumla
Rauhia ameyazangumza hayo wakati akiwalemisha wanafunzi wa kidato cha tatu skuli ya sekondari ya kinyasini iliyopo wilaya ya kaskazin A unguja mkoa wa kaskazini Unguja katika wiki ya kisheria Zanzibar.
Amesema lengo na kufika kwa wanafunzi hao ni kuhamasisha wanafunzi mashuleni wajiekee malengo ya kimasomo na kuepuka vishawishi na kujikita katika matumizi sahihi ya mitandao kwani mitandao hiyo inafaida kubwa ikiwa vijana wataelimishwa na kufahamu faida ya mitandao katika harakati zao za masomo kwani wengi baadhi yao hawatambui matumizi sahihi ya mitandao na hutumia vibaya mitandao hiyo na hatimaye sheria uchukua mkondo wake pale kijana au mtu yoyote atafanya kosa la kimtandao katika nyanza mbali mbali.
Hivyo amesema ni jukumu la serikali, taasisi mbali mbali na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kuweelimisha wanafunzi na vijana kwa ujumla ili mitandao iweze kuwa ni fursa bora kwao katika kufanikisha mambo yenye tija kwa maslahi ya wanafunzi na taifa kwa ujumla.
Pia amewasisitiza wanafunzi kuwa na nidhamu na bidii katika masomo na kuwatii wazazi, walimu na jamii kwa ujumla pamoja na kushirikiana katika masomo ili wafanye vyema katika mitihani yao na kuendelea na elimu ya juu kwa misingi ya kujijengea maisha bora kwa maendeleo yao,familia na taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya Mwalimu mkuu skuli hiyo Mwalimu Moh'd Bakar Sharif amesema kulingana ukuaji wa kasi kwa teknolojia dunia elimu hiyo ni wakati sahihi kwa upande wa wanafunzi kuelimishwa kwani itawasaidia katika nyanza mbali mbali za masomo yao na kuweza kuzikimbilia fursa mbali mbali zilipo katika mitandao ulimwenguni.
Hivyo amewashauri ofisi ya mahakama na taasisi mbali mbali kuendeleza mwenendo wa huo ili kuwajengea wanafunzi na vijana kwa ujumla uwelewa mpana wa matumizi sahihi ya mitandao kwa lengo la kuweza kufika ndoto zao za masomo na kimaisha.
Hassan Ali Khamis na Shawana Buhet Kher ni miongoni mwa wanafunzi walioshiriki katka mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo wameyapokea kwa hali za kuvutiwa nayo kwani walikuwa baadhi ya Mambo katika mitandao hawajui kama ni makosa kisheria hivyo kupitia elimu waliyo patiwa wameelimika kwa kiasi kikubwa na wameahidi kuyazingatia na kuyafanyi kazi yale yote waliyopatiwa kwa misingi ya maendeleo yao ya kimasomo ma kimaisha kwa ujumla.


