Wilaya ya kaskazin A unguja.
Jumuiya ya wazaz wilaya ya kaskazini A Unguja leo imefanyika ziara ya kuwatembelea wanafunzi wa kidato cha nne, tano na sita skuli ya sekondari mkwajuni na mkokotoni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kwa lengo la kuwahamasisha kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linalo tarajiwa kuanza tarehe 22 hadi 24 Februari 2025.
Akizungumza na wanafunzi hao mwenyekiti wa jumuiya wazazi Hamad Makame Juma amesema jumuiya hiyo inajukumu katika suala la elimu,malezi,utamaduni na mazingira hivyo ujio wao miongoni mwa majukumu yao katika ujenzi wa maendeleo ya chama katika jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu wa jumuiya hiyo Jafar Moh'd Khamis amesema lengo la ziara hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hao waliofika miaka 18 na kuendelea kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura awamu ya pili linalo tarajiwa kuanza hivi karibuni hivyo nafasi hiyo ya kikatiba ni muhimu kwako kushiriki kwa aslimia zote kwa wale wote waliokidhi vigezo vyote vya kisheria.
Amesisitiza kujiepusha na watu maneno ya upotishaji wenye nia mbaya za kimaendeleo nchni bali wawe mbele katika kujitokeza kujiorodhesha taarifa zao na kuwa mabalozi kwa wengine mitaani juu ya zoezi hilo kwa misingi ya kupata haki zao za msingi na kushiriki ipasavyo oktoba 2025 katika uchanguzi mkuu nchini.
Amesema jumuiya na chama kwa pamoja kitaendelea kuunga mkoa juhudi za maendeleo za marais wote nchini hivyo ni vyema wanafunzi hao wakatunza miundombinu ya elimu na kujitahidi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ya maisha.
Nao wanafunzi Asia Musa Ali na Ibrahim Haji Haji wamesema wanashukuru kwa elimu na uhamasishaji wa zoezi hilo kwani mengi walikuwa hwajui hivyo wameahidi kuyazingatia na kuyafanyia kazi yale yote yaliyo elezwa kwa maslahi yao wakiwa vijana na taifa kwa ujumla.


