Popular services

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUFANYA UCHECHEMUZI WA MASUALA YA AFYA YA UZAZI KATIKA JAMII


Na,Nishan khamis. 
Zanzibar.

Waandishi wa habari Zanzibar wamehimizwa kutumia kalamu zao ipasavyo katika kufanya uchechemuzi wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kufahamu na kuzingatia elimu ya afya ya uzazi na kudumisha lishe bora ili kujikinga na maradhi mbali mbali kwa misingi ya kupeleka mbele maendeleo ya jamiii na taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema Daktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi Dkt Ummukulthum Omar Hamad kutoka hospital ya Rufaa ya Mnazi mmoja wakati akizungumza katika semina ya mafuzo ya siku mbili yaliyo andaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZANZIBAR juu ya kuwajenga uwezo waandishi wa habari 27 kutoka Unguja katika kufanya uchechemuzi wa masuala ya elimu ya afya ya uzazi katika jamii. 

Dkt Ummukulthum,amesema bado kuna tatizo kubwa la ulewewa mdogo katika jamii hasa vijana katika suala la afya uzazi jambo ambalo linapelekea uwepo wa mimba zisizo tarajiwa,mimba za utotoni, ukosefu wa Kizazi, ongezeko la virus vya UKIMWI, hivyo ni vyema vyombo vya habari kutimiza wajibu wao kwa kushirikiana na wizara ya afya, madaktari na wanaharakati katika kuisadia jamii nama ya utambuzi wa afya ya uzazi kwa maslahi ya jamiii na taifa kwa ujumla.


Awali akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya mkurungezi wa TAMWA-ZNZ,Tatu Ali Makame amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa wanahabari kwa kuwajengea uwelewa wa masuala ya afya ya uzazi hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiaisi kikubwa katika kuelimisha jamii katika masuala hayo, amewanasihi wanahabari hao kutumia nafasi hiyo katika kuleta mabadiliko juu ya afya ya uzazi katika jamii. 

Nae, Afisa Programu na afisa mawasiliano TAMWA-ZNZ Khairat Ali amesema mafunzo hayo kwa wanahabari yana lengo la kuwajengea uwelewa katika juu ya haki ya afya ya uzazi ili wafanye uchechemuzi katika masuala hayo katika maeneo ya uzazi wa Mpango, saratani ya kansa ya kizazi, HIV pamoja na ushiriki wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi hivyo wanahabari kupitia kalamu zao zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuisadia jamaniii katika utambuzi wa masuala hayo.

Mwanaharakati wa masuala ya UKIMWI Zanzibar Dkt Sihaba Saadat ambaye ni miongoni mwa wakufunzi katika mafuzo hayo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na tume ya taifa ya UKIMWI imeonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU Zanzibar mwaka 2023 wanao ishi na VVU Zanzibar ni 0.4% ,ambapo mkoa wa Kusini Unguja wanao ishi na VVU ni 0.8%,kaskazini Unguja 0.7%,Mjini Magharibi 0.4%,Kaskazini Pemba 0.2% na kusini Pemba ni 0.5% tafiti zikionesha kuwa wanawake hupata maambukizi mara mbili zaidi ya wanaume(42,000 vs18,000) ikiwa waathirika wakubwa ni wanawake wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24, ivyo amewasisitiza wanahabari kutumia kalamu zao katika kuelimisha jamiii njia za kujikinga na maradhi ya UKIMWI. 

Akitilia mkazo katika uwajibikaji wa wanahabari, mwanahabari mkongwe Zanzibar Dk Imane Duwe amewasisitiza wanahabari hao kufuata maadili na misingi ya habari katika majukumu yao ili kufanya kazi iyo kwa weledi zaidi katika kuisadia jamii kufahamu, kuzingatia na kuyafanyia kazi masuala ya afya ya uzazi, liche bora na maradhi ya UKIMWI ili kuwa na taifa lenye watu wenye afya imara na bora kwa maendeleo ya jamiii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Abdul-Kadir Sakaza mwandishi wa habari kutoka Tumbatu fm na Berema Suleiman Nassor kutoka Zenji Fm wamesema wanawashukuru TAMWA-ZNZ kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yamewajengea uwezo mzuri katika utambuzi wa masuala mbali mbali ya afya ya uzazi, na lishe, hivyo ikiwa wao ni muhimili mkubwa katika dunia watatumia kalamu zao vizuri katika kuelimisha jamii juu ya masuala ya hayo.