Mkoa wa Kusini Unguja.
Chama kikuu cha wavuvi wadogo wadogo Zanzibar(ZASFICU) leo kimetoa msaada wa vifaa kwa wakulima wa mwani 36 kwa wanakjiji cha Muungoni kilichopo wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja
Akizungumza katika Hafla hiyo mwenyekiti wa zasficu Maalim Omar Moh'd Ali amesema miongoni mwa changamoto zinazo wakabili wakulima wa mwani ni ukosefu wa vifaa vya kiusalama katika ufanyaji wa shughuli zao hali inayopelekea mara kwa mara kupata athari za majeraha katika miili yao.
Amesema zasficu inatambua changamoto hizo na wameona kuna kila sababu ya kuwapatia vifaa hivyo ili viwasaidie kuwa salama zaidi katika uzalilishaji wa mazao yao ili waepukane na athari wanazo zipata katika shughuli hizo.
Amesema zasficu wataendelea kuunga mkono juhudi sera za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi pamoja na uwepo wa sera ya uchumi wa buluu na uvuvi hivyo utoaji wa vifaa hivyo vikiwemo viatu na gloss walizo patiwa wakulima hao ni mwanzo na itakuwa ni muendelezo ili kuwalinda na kuwa salama zaidi ili wazalishe mazao mengi zaidi kwa maisha bora ya wakulima na wavuvi nchini ikiwa ni miongoni mwa malengo ya uwepo wa zasficu pamoja na kuwa na sauti moja ya utetezi kwa maslahi ya maisha bora ya wavuvi wadogo wadogo na wakulima wa mwani nchini.
Mkurungezi wa kamati ya mipango,miradi na ubunifu kutoka zasficu Mzee Said Dahoma amebainisha kuwa zasficu imeanza kubuni miradi mikubwa ya kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo na wakulima wa mwani ili kukuuza uzalilishaji wao kwa wingi na obora zaidi ili kukuza pato lao kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Mzee amesema msaada wa vifaa hivyo ni hatua ya mwanzo ambapo vimegahaimu shilingi laki nane kwa hisani na Bwana Yoland Brown kutola nchini England kwa kushirikiana na zasficu katika kutatua changamoto za wavuvi wadogo wadogo na wakulima wa mwani ili kuendelea kuwajengea mazingira bora ya ufanyaji wa shuguli zao kwa misingi ya kuwainua kiuchumi na kuwa maisha bora kama wafanyakazi wengine nchini.
Kwa upande wake sheha wa shehia ya Muungoni Musa Juma Mbwato amewashukuru ZASFICU kwa msaada huo na amewaomba kuendelea na zoezi hilo kwani katika kijiji chake kuna watu 315 wanao jishughurisha na ukulima wa mwani hivyo ameomba zoezi hilo liwe endelevu ili na wakulima wengine wanufaike na vifaa hivyo katika shughuli zao za ukulima wa mwani.
Nao baadhi ya wakulima wa mwani walio kabidhiwa vifaa hivyo akiwemo Issa Khamis na Hidaya Suleiman wametoa shukrani kwa ZASFICU kwa kuwathamini na kuwajali kwa kuwapatia msaada huo kwani walikuwa wakikabiliwa na athari nyingi zikiwemo vya kutobolewa miguuni na mawe, samaki na vitu mbali mbali vilivyo kuwa vikiatarisha usalama wao wakati wa shughuli zao za ukulima wa Pwani.
Walibainisha kuwa hufika wiki nzima baadhi yao hushundwa kwenda katika shughuli zao kutokana na kupata madhara hayo hivyo ujio wa vifaa hivyo ni faraja kwao kuwa salama zaidi katika shughuli zao za uzalilishaji wa mwani.
Hata hivyo wameiomba serikali kuangalia soko zaidi la mwani hasa katika kumkomboa mwanamke kiuchumi kwani kwa upande wao wamezalisha mwani mwingi ila soko hakuna ,pia wameziomba taasisi mbali mbali kwa kushirikiana na wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi na ZASFICU ziendelee kuwasaidia katika kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli hizo.




