Wilaya ya Kaskazini A Unguja .
Mbunge wa jimbo la Kijini wilaya ya Kaskazini A Unguja Mhe Yahya Ali Khamis(Mambalesi) amekabidhi vifaa mbali mbali vya hospital vikiwemo vitanda vya kisasa vya kulalia wagonjwa,baskeli za watu wenye ulemavu,magodoro,mashine za kisasa,mashuka, nguo na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni mia sita za Kitanzania ikiwa ni msaada kutoka taasisi ya Human bridge kutoka nchini Sweden.
Mbunge Mambalesi amayasema hayo hapo jana katika hafla ya kumkabidhi vifaa hivyo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la kijini,amesema ufadhili huo unatokana serikali ya Sweden mara baada ya kukutana na balozi wa Sweden na kumueleza changamoto mbali mbali zilizopo katika jimbo lake kutokana na ukosefu wa vifaa mbali mbali za hospital zilizopo katika jimbo hilo.
Hivyo alieleza kutokana na jitihada zake za kuwatafutia wananchi wake misaada mbali mbali katika bara la ulaya balozi wa Sweden kupitia mkurungezi wa Human bridge Sweden wametoa msaada huo wa vifaa ikiwa ni mwanzo wa kuendelea kuisadia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya hospital nchini kote ili kuondoa changamoto izo kwa wananchi kwa misingi bora ya maendeleo ya kiafya nchini.
Amesema ikiwa yeye ni kiongozi wa jimbo hilo ana kila wajibu wa kuwasaidia wananchi wake kwani jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo yenye hali duni ya kimaisha hivyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake jimbo hilo,wadau mbali mbali wa maendeleo na serikali kwa ujumla wataendelea kuimarisha miundoni mbali mbali ya kimaendeleo katika jimbo hilo huku akiwahakikishia kutekeleza ahadi yake ya Ambulance katika jimbo hilo.
Pia Mbunge amewasisitiza wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husein Ali Mwinyi kwa jitihada kubwa za kimaendeleo zinazo endelea nchini katika kuimarisha maisha bora ya watanzania.
Ameeleza kutoka na mchango wake huo amechaguliwa kuwa balozi wa human bridge Sweden hapa Tanzania katika kusimamia vifaa vyote vya hospital vitakavyo letwa nchini kutoka Human bridge Sweden ikiwa ni mikakati mizuri ya kuendelea kuimarisha ushirikiano mzuri wa Sweden na Tanzania katika masuala ya upatikanaji wa vifaa vya hospital.
Akizungumza katika shughuli hiyo mstahiki Meya baraza la Manispaa wilaya hiyo Machano Fadhil Machano(Babla) amempongeza mbunge kwa jitihada kubwa za kutafuta ufadhili wa vifaa hivyo vyenye thamani kubwa ambavyo vitawasaidia katika kuimarisha maendeleo ya upatikanaji wa hudumu bora za kiafya nchini.
Babla amesema kutokana na kasi kubwa ya uimarishaji wa miundombinu ya kiafya nchini chini ya Rais Dkt Husein Ali Mwinyi ni utekelezaji mkubwa wa ilani CCM ya mwaka 2020-2025 hivyo ni vyema wananchi na madaktari wakavitunza vifaa hivyo ili viendelee kudumu kwa muda mrefu kwa maslahi mapana ya taifa.
Amesema kwa niaba ya serikalini ya mapinduzi ya Zanzibar wanatoa shukrani za dhati kwa Human Bridge kutoka kutoka nchini Sweden kwa msaada huo na amewahakikishia kuendelea kushirikiana nao katika kujenga maendeleo endelevu nchini.
Kwa upande wake mkurungezi mtendaji wa human bridge Sweden Bahat Kitoh ametoa shukran za dhati kwa watu wa Zanzibar na mbunge wa jimbo hilo kwa kuendelea kutafuta njia mbali mbali za kutatua changamoto za jimbo lake ikiwa ni uongozi wenye faida sana kwa maendeleo ya taifa.
Kitoh amesema mara baada ya ujio wa mbunge huyo nchini Sweden na kukutana na balazo na kueleza changamoto zake kupitia serikali ya nchi hiyo imeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwasaidia vifaa hivyo kwa misingi ya kuendelea kuunga mkono juhudi za rais Dkt Mwinyi za kuimarisha miundoni mizuri ya kiafya nchini.
Amesema kutoka na kasi ya maendeleo yanayo endelea nchini chini ya rais Dkt Mwinyi wataendelea kuleta vifaa vingi vya matibabu vya hospital zote za Zanzibar wiki ijayo ambapo kwa upande wa Tanzania bara washapeleka kontena 40 zenye vifaa vya hospital ili kuunga mkono pia juhudi za maendeleo nchini Tanzania chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.
Nae msaidizi Daktari zamana hospital ya wilaya Kivunge Daktari Tamimu Hamad Said amese ujio wa vifaa hivyo vya kisasa na vyenye thamani kubwa ni faraja kwako kutoka na hospital hiyo kuwa na uhitaji kutoka na kuhudumia wagonjwa kutoka wilaya hiyo,mkoa huo na nje ya mkoa kwa sasa hivyo ametoa pongezi za dhati kwa wafadhili na mbunge kwa kazi kubwa aliyoifanya katika jimbo lake na ameahidi kusimamia vifaa hivyo ili vidumu kwa muda mrefu zaidi.
Aziza Moh'd Salum ni miongoni mwa wananchi waliohudhuria katika hafla iyo amesema amemshukuru kwa kiasi kikubwa kwa ujio wa vifaa kwani vitawasaidia katika hospital yao hasa wanawake na watu wenye ulemavu hivyo ametoa kwa pongezi kwa wafadhili na mbunge wa jimbo hilo kwa kazi kubwa aliyoifanya mpaka kufika vifaa hivyo katika hospital ya kivunge.




