Na,Nishan khamis.
Kidoti
Katibu Tawala Wilaya ya Kaskazini A Unguja Maryam Said Khamis leo amekabidhi vifaa mbali mbali vya maji kwa wanakijiji cha kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja mkoa wa kaskazini Unguja kwa misingi ya kuimarisha miundoni ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji hicho.
Katibu Tawala ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanakijiji wa kidoto katika hafla hiyo ambapo amewataka kuuitunza Miundo Mbinu ya maji ili kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu na huduma ya maji safi na salama inapatikana kwa wakati ili kuondoa changamoto iyo hasa kwa wakina mama na watoto wa kike wanao sumbuka zaidi katika uchotaji maji sehemu za mbali.
Aidha amesema serikali ya wilaya inaunga mkono juhudi za rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt Husein Ali Mwinyi katika harakati zote za kuboresha Miundo Mbinu mbali mbali hivyo ni vyema jamii ika thamini na kuitunza Miundo hiyo ili idumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya jamiii na taifa kwa ujumla.
Amebainisha kuwa zaidi ya shilingi milioni saba zimetumika katika maendeleo ya shehia hiyo katika uimarishaji wa miundombinu ya maji kwa ununuzi wa mipira ya sambazaji wa maji,Pampu mbili za kisima pamoja na tangi la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita elfu tano.
Nae, Sheha wa shehia hiyo Hamad Makame Hamad ameishukuru Serikali ya Wilaya kwa juhudi zao za kuwatatulia Changamoto zinazowakabili, hivyo ameiomba Serikali hiyo kuendelea kuwapatia wafadhili wengine ili kuwasaidia katika kukuza maendeleo ya Shehia.
Aidha amesema atahakikisha anashirikiana na wanakijiji katika kutunza miundo mbinu hiyo ili ielendelee kudumu kwa muda mrefu kwa maslahi zaidi ya kijiji hicho na vijiji vya jirani.
Kwa upande wao Wananchi waneahidi kuilinda na kuitunza Miundo Mbinu ya Maji ili kuendelea kuwasadia katika haraka zao za Maisha, kwani upatikanaji wa Maji itawasaidia katika kilimo na shughuli mbali mbali.