Mkwajuni, wilaya ya kaskazini A Unguja.
Umoja wa makundi ya sanaa wilaya ya kaskazini A Unguja(UMASAKA) wamehimizwa kutumia sanaa zao kwa kuibuna vibaji pamoja na kuwa na mikakati madhubuti kwa misingi ya maendeleo ya wasanii wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema hapo jana Afisa Habari wilaya ya kaskazini A Unguja Salum Sadoun wakati akizungumza na makundi mbali mbali ya wasanii wilaya hiyo katika uchanguzi mkuu uliofanyika kituo cha walimu mkwajuni wilaya ya kaskazini A Unguja Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Sadoun amesema ikiwa wasanii watakuwa na sauti moja kwa ushirikiano wa hali na mali ni njia moja wapo ya kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kupitia sana zao,hivyo ni vyema mashirikiano ya dhati yakawepo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Halikadhalika amewasisitiza kuelekea uchaguzi mkuu ni vyema wakatumia sanaa zao kuhubiri amani,upendo na mshikanamo ulipo nchini ili kufanikisha zoezi la uchanguzi oktoba 2025 likafanyika kwa amani na utulivu kwa maslahi mapana ya taifa.
Mwenyekiti mkuu mpya wa UMASAKA Mustapha C.Markus amesema atahakikisha anashirikiana ipasavyo na wanachama wenzake katika kuleta mabadiliko yenye tija ya sanaa katika wilaya hiyo kwa maendeleo ya UMASAKA na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria tukio hilo wamesema miongoni mwa changamoto zinazo wakabili ni ukosefu wa elimu ya sanaa miongoni mwao ni tatizo kubwa linalo kwamisha kufikia malengo yao,hivyo wameomba ushirikiano kwa wadau mbali mbali kushirikiana nao katika maendeleo ya sanaa hasa kwa vijana ikiwa ni nyezo muhimu ya ajira kwa vijana nchini.




