Popular services

ZYF KUWASAIDIA VIJANA KATIKA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO


Mratibu ZYF Abdallah Hijja akizungumza na Vijana katika mafunzo ukumbi wa kidongo chekundu.

Jukwaa la Vijana Zanzibar ZYF limekamilisha mafunzo ya siku tatu ya kuwafundisha vijana mbalimbali katika jamiii na vyuo vikuu juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Nishani Blog Mratibu wa Mradi wa kuwawezesha vijana kujua matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ikwemo Whatssap Facebook,Tweeter,Tiktok na mengine ili kuepuka kuingia katika uvunjaji wa sheria za mitandao.

Mradi huo unaotarajiwa kuwafikia zaidi ya vijana elfu mbili Zanzibar upo chini ya ufadhili wa International Media Support IMS utadumu kwa zaidi ya miezi 8.

Na  Nishani Khamis Blog.